SINEMA YA FARU JOHN YAFIKIA SEHEMU HII,SERIKALI YAIBUKA YAPIGA MARUFUKU ,SOMAHAPO KUJUA
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani
amesema kuwa hakuna mwenye Mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusu faru John
kwa sasa zaidi ya Waziri Mkuu kwa kuwa jambo hilo liko chini ya ofisi yake.
kwaajili ya uchunguzi.
Ameyasema hayo Wilayani Ngorongoro katika ziara yake
ya kikazi ya siku mbili wilayani humo kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja
na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyo yatoa hivi karibuni akiwa
Arusha.
“Ripoti hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakae
weza kutoa ripoti hii nje kwaajili ya matumizi ya kila mmoja wetu kwa maana ya
mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine ya serikali yenye uhalali wa kutoa
tamko au ufafanuzi wa jambo hili.”amesema Makani.
Hata hivyo, Makani amesema kuwa wanasubiri maagizo
au maelekezo na mwelekeo wa sasa juu ya jambo hilo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.