Takwimu
za ukuaji wa uchumi nchini unaonyesha unaendelea kukua kwa kiasi kubwa zaidi
kulinganisha na mataifa mengine na kuwa miongoni mwa Nchi za
bara la Afrika , Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakuwa
ikifuatiwa na Congo DRC na Rwanda,Kenya, Uganda, Burundi, Afrika ya Kusini,
Zambia na Malawi.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa fedha na Mipango Dkt Phillip
Mpango amesema kuwa kukua kwa uchumi kunapimwa kwa kuangalia shughuli
mbalimbali za kiuchumi zikiwemo ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao
mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi, uzalishaji wa bidhaa za viwandani na
migodini, ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali za kwa jamii
ikiwemo afya, elimu na maji.
"Kasi ya kuongezeka au kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma katika
nchi ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa
Taifa kwa ujumla ambapo kiashiria kimojawapo kinachotumika kupima ukuaji wa
uchumi ni ukuaji wa pato la Taifa."
Aidha Dkt Mpango ameongeza kuwa kiashiria kingine ni mfumuko wa bei bao unapima
mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya ambapo ulipungua
kutoka asilimia 6.5 januari 2016 hadi asilimia5.5 juni na kupungua zaidi
hadi kufikia asilimia 4.5 na kupanda hadi asilimia 4.8 mwezi novemba 2016.
Amesema katika mwezi huo wa Novemba takribani nchi zote zilikuwa na ongezeko la
mfumuko wa bei kutokana na kuyumba kwa ugavi wa chakula katika nchi ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki na kupanda kwa bei kwa bei za mafuta katika soko la Dunia.
Dkt Mpango amesema kwa tathimi ya upande wa mabenki unaonyesha kuwa benki
yanaendelea kuimarika huku yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha kwa kuangalia
uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana
zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi ambao ulikuwa kwa asilimia 37.46
ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20.
" amana za wateja katika benki zilipungua kidogo kutoka Trilioni 20.73
mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi Triliani 20.57 mwezi septemba kutokana na
uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya Umma
kutoka benki ya biashara kwenda benki kuu ya Tanzania."
Hata hivyo Mpango amesema kwa kuzingatia mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa
kipindi cha Januari hadi septemba 2016 matarajio ni kwamba kasi ya ukuaji wa
uchumi kwa mwaka 2016 na 2017 unatarajiwa kufikia hadi asilimia 7.2 kama
ilivyokaririwa awali.
SERIKALI YAENDELEA KUJITETEA KUHUSU HALI YA UCHUMI,YASEMA BADO UCHUMI UPO VIZURI,SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
20:47:00
Rating: 5