Zinazobamba

TUKIO KUBWA ALILOFANYA MEYA WA KINONDONI LEO,SOMA HAPO KUJUA


 Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni Benjamini Sitta akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kusaini mkataba huo jijini dar es salaam,kushoto ni mhandisi wa manispaa hiyo Abdul  Digaga


Halmashauri ya manispaa ya kinondoni imezindua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji  wa jiji la dar es salaam kwa kusaini mkataba wenye thamani ya bilioni 22 na mkandarasi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.

Akizungumza na waandishi wa habari maeneo ya makumbusho kata ya kijitonyama  leo,Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sitta amesema kuwa mpango  wa mradi huu unalenga  kuboresha miundombinu ya barabara ambayo   itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na  kuongeza thamani ya makazi ya watu pamoja na kupinguza umaskini.

"Katika uboreshaji wa miundombinu barabara zitajengwa kwa lami nzito na huduma  nyingine za watumiaji wa barabara kama maeneo ya waendao kwa miguu,taa  za barabarani,mitaro ya majia pamoja na alama za vivuko ambavyo  vitambadilisha sura ya manispaa ya Kinondoni na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla."


Aidha meya ametaja  barabara  ambazo Zitahusika katika mpango huu ni pamoja na soko la makumbusho  km1.45,MMK km 0.9,Nzasa km 1.25, Viwandani km 1.68 na Tanesko soko la
samaki ambazo zitajengwa ndani ya mwaka mmoja na kwa kiwango  cha juu.

Kwa upande wake mkandarasi kutoka Estim Construction Jagdish Bhudia amesema kuwa watajenga barabara kwa kiwango kinachotakiwa kama kwa kutumia lami
nzito ili ziweze kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.

Hata hivyo mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni ameongeza kwa kuwataka wanachi wote wa manispaa hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi
huu ambao unalenga kuboresha miundombinu  na kuimarisha huduma za  kiuchumi, kibiashara na kijamii.