SERIKALI YA MAGUFULI HOI,WAZIRI WAKE ATISHIKA,SOMA HAPO KUJUA
Maduka yakiwa yamefungwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mdororo wa uchumi |
MAMBO yanakwenda mrama. Ndivyo unavyoweza kusema
baada ya Dk. Philipo Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango kuingia kiwewe kutokana
na maduka kufungwa kwa kasi, anaandika Faki Sosi.
“Sielewe
ni nini” ni kauli ya Dk. Mpango mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam
alipozungumzia hali ya uchumi kuanzia Julai mpaka Disemba mwaka huu na
matarajio ya mwaka 2017.
Kuyumba kwa biashara kumesababisha zaidi ya maduka
1,800 kufungwa ndani ya miezi mitatu.
Amethibitisha kwamba, mapato yaliyokuwa yakipatikana
kutokana na biashara ya maduka ya jumla na rejareja yamepungua kutokana na
maduka hayo kufungwa yakiwemo 1,872 baada ya kuyumba kibiashara.
Wilaya zenye maduka hayo zilizoathirika kutokana na
kuyumba kwa biashara jijini Dar es Salaam ni pamoja na Kinondoni ambapo maduka
443 yamefungwa, Temeke (222), Ilala (1,076) na Arusha 131.
Kwa kauli ya Dk. Mpingo, miongoni mwa maduka
yaliyofungwa ni yale yaliyokuwa yakifanya biasahra za jumla na rejareja,
yanayojihusisha na vyombo vya usafiri pamoja na vifaa vya ujenzi.
Amesema kuwa, mpaka sasa hakuna utafiti wowote
uliofanyika ili kubaini sababu za maduka hayo kufungwa na kwamba, hisia
zinazotawala ni kuwepo kwa changamoto katika kuyaendesha.
“Sababu hasa za biashara hizo kufungwa hazijabainika
kutokana na ugumu wa kupata taarifa hizo kutoka kwa wenye biashara
zilizofungwa,” anasema.