MAKADA WA CUF WAMUANGUKIA MAALIM SEIF WATAKA AKAE CHINI NA PROFESA LIPUMBA,SOMA
NA KAROLI VINSENT
MAKADA wa chama cha Wananchi (CUF) ambao wanaumuunga
mkono mwenyekiti wa Chama hicho ambaye anatambulika na ofisi ya msajili
nchini,Profesa Ibrahim Lipumba , wamemtaka Katibu mkuu wa Chama hicho,Maalim
Seif kumaliza tofauti zao na Lipumba ili
kuweza kukinusuru chama hicho kupagalanyika.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Aliyekuwa
mkurugenzi Taifa wa Ulinzi wa (CUF),Thinex Muhamed wakati akizungumza na
waandishi wa habari Makao mkuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni,
Ambapo Kada huyo amesema kwa sasa anaona chama chake
hicho kinazidi kwenda vibaya kutokana na kuwepo mgogoro mkubwa kati ya upande wa
Katibu na Mwenyekiti jambo analodai litawakatisha tama wanachama na wananchi
kuwa na imani na CUF.
“Kikweli mgogoro huu unakifanya chama chetu kukosa
nguvu na kuwafanya wananchi kuanza
kukosa imani nasi,leo ukiangalia katika pande hizi mbili zinazofutana kwa
upande wa Maalim Seif yeye ananguvu kubwa upande wa chama Visiwani Zanzibar na
profesa Lipumba ananguvu kubwa huku bara yote haya yanakifanya chama chetu kuwa
na mgogoro’amesema Muhamed.
Amesema Njia pekee ya kuweza kumaliza mgogoro huo ni
kwa pande mbili zinazotofautiniana na kukaa pamoja na kuweza kukijenga chama.
“Leo mgogoro
huu hauwezi kumalizika bila ya pande mbili hizi zinazotofautiana kukaa
pamoja,na namuomba Maalim Seif arudi ofisini na kukaa meza moja na Lipumba ili
tofauti zote ziishe tujenge
chama”amesema
.Hata hivyo,Muhamed amesema hata vitabu vitakatifu
vinasema binadamu wasamehane pindi wanapokoseana huku akizitaka pande hizo
kutumia hoja hiyo kusameana na kukijenga chama hicho.
Kauli ya Kada huyo mkongwe wa chama hicho inakuja
ikiwa teyari chama hicho kinaaingia kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Diwani
huku visiwani Zanzibar ambapo chama hicho kitamsimamisha mgombea mmoja huku
akiungwa na vyama vinavyounda mkono muunganiko wa UKAWA.
Mbali na uchaguzi huo teyari chama hicho kimekiachia
chama cha Demokrasia maendeleo Chadema kwenye marudio ya kata zaidi ya 20
kwenye uchaguzi huo wa marudio kwenye ngazi ya udiwani.