SHEIKH PONDA USO KWA USO NA WAZIRI MKUU MAJALIWA-MATUKIO KATIKA MWAKA 2016
Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa, amewataka
waumini wa dini ya Kiislamu kuitumia sikukuu hii ya Idd el Haji kutenda
mema na kuungana na waumini wengine katika kudumisha amani ya nchi yetu.
Waziri
Mkuu akiyasema hayo leo Septemba 12, 2016, kwenye ibada ya sala ya Idd
el Haji iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke, jijini Dar
es Salaam ambapo miongoni mw masheikh maarufu walihudhuria ibada hiyo
ni pamoja na Sheikh Shariff, Sheikh Nurdin Kishki,(mwenyeji wa hadhara),
Sheikh Ponda Issa Ponda na Sheikh Rajab Katimba.
â€Å“Kwa
niaba ya serikali yenu, nawatakia sikukuu njema, na ninaomba
kuwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, pamona na Makamu wa Rais, Mh.
Samia Suluhu Hassan, na niwaombe ndugu zangu muitumie sikukuu hii
kudumisha amani na upendo,†alisema Waziri
Mkuu.
Waziri Mkuu pia alitumia fusa hiyo kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu
kote nchini, kuwaombea wananchi wa mkoa wa Kagera waliopatwa na maafa
ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo.
Waziri
Mkuu ambaye alihudhuria ibada ya kuaga miili ya watu 16 kwenye uwanja
wa michezo wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera Jumapili Septemba 11,
2016, alisema kwa sasa kuna majeruhi zaidi ya 100 ambao bado wanapatiwa
matibabu.
Tetemeko hilo lilillopelekea uharibifu mkubwa wa nyumba lilitokea Jumamosi alasiri Septemba 10, 2016.
Naye
mwenyeji wa Ibada hiyo Sheikh Nurdin Kishki, alimshukuru Waziri Mkuu
kwa kuungana na waumini wa dini ya Kiislamu wa Wilaya ya Temeke, katika
swala hiyo ya Idd. â€Å“Nduhgu zangu napenda nimshukuru Waziri wetu Mkuu
kwa kutoka Oysterbay hadi kufika huku Temeke kuungana nasi katika
kutekeleza swala hii ya Idd El Haji, mwenyezimungu amjalie heri na
busara katika uongozi wake,†Alsiema Sheikh Kishki.
Na Khalfan Said – K-VIS Blog
 Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
 Sheikh Shariff akiongoza Swala ya Idd El Haji viwanja vya Mwembe Yanga , Temeke jijini Dar es Salaam
Muumini wa Kiislamu akiomba dua
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeana mikono na Sheikh Ponda Issa Ponda, mara baada ya swala hiyo
 Waziri Mkuu, akiteta jambo na sheikh Ponda
 Waziri Mkuu, akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Shariff, (kushoto), na Sheikh Nurdin Kishki
 Waumini wa Kiislamu wakiwa kwenye swala
 Waumini wa Kiislamu, wakiomba dua
 Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na
Masheikh na viongozi wa serikali mara baada ya swala hiyo
 Sheikh Nurdin Kishki, akisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
 Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa
swala ya Idd El Hajji viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es
Salaam
 Sheikh Nurdin Kishki, kiwahutubia waumini wa dini ya Kiislamu kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga, wakati wa swala hiyo
 Watoto
hawa wa Kiislamu, wakionyesha furaha baada ya kushiriki swala ya Idd El
Hajji, (Mlulu Khalfan (kushoto) na mdogo wake Kuugara.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Sheikh Mkuu na Mufti
wa Tanzania, Alhaj Abukary Zubeiry Bin Ally baada ya kuwasili Shelui
mkoani Singida kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12, 2016.
Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi. (PICHA NA OFISI YA
WAZIRI MKUU)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Baraza la Maulid
lililofanyika kitaifa, Shelui, Singida Desemba 12, 2016
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akizungumza katika Baraza
la Maulid lililofanyika Shelui mkoani Singida ambapo mgeni rasmi alikuwa
ni Waziri Mkuu, Kassim Majalaiwa , Desemba 12, 2016
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Alhaj Abubakary
Zubeiry bin Ally akizungumza katika Baraza la Maulid lililofanyika
kitaifa Shelui mkoani Singida na mgeni rasmi alikuwa ni Waziri Mkuu, Kassim
Majliwa
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo katika kijiji cha
Shelui mkoani Singida, Desemba 12, 2016
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo katika kijiji cha
Shelui mkoani Singida, Desemba 12, 2016
Baadhi ya washiriki wa Baraza la Maulid wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo katika kijiji cha
Shelui mkoani Singida, Desemba 12, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya
Ndani, Mwigulu Nchemba baada ya kuwasili Shelui mkoani Singida kuwa
mgeni rasmi katika Baraza la Maulid Desemba 12, 2016. Kulia ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba. Muungano na Mazingira
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dkt. Rehema Nchimbi baada ya kuwasili Shelui kuwa mgeni rasmi katika
Baraza la Maulid, Desemba 12, 2016