SAKATA LA MASHUSHU WA TANZANIA KUTEKWA NCHINI MALAWI YAISHUTUA SERIKALI,SASA WAAPA KUCHUNGUZA,SOMA HAPO KUJUA
Serikali inafanya uchunguzi kuhusu tuhuma
zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Malawi kuwa vimewakamata ‘mashushu’
nane wa Tanzania wakijaribu kuingia kinyamela kwenye mgodi wa ‘uranium’.
Taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini
humo juzi zimedai kuwa watu hao nane walikuwa wapelelezi na kwamba walitaka
kuingia kwenye mgodi huo kujaribu kuchunguza kama nchi hiyo inatengeneza
‘nyuklia’ katika eneo la Kayerekera. Ripoti iliyowekwa kwenye mitandao
mbalimbali ya Malawi pia imedai kuwa watu hao waliingia nchini humo bila kuwa
na nyaraka za kusafiria.
Akizungumzia madai hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga jana alifanya mahojiano
na The Citizen na kueleza kuwa hakuwa na taarifa hizo lakini atazifuatilia kwa
kina na kufanya uchunguzi kwani ni tuhuma kubwa na nyeti.
“Ndio ninasikia hilo kwa mara ya kwanza kutoka
kwako. Hizi ni tuhuma kubwa, nitafuatilia kwa kina leo (jana) jioni kwa
kuwasiliana na ubalozi wetu wa Malawi kufahamu kama wanafahamu lolote kuhusu
hili,” Dk. Mahiga anakaririwa.
Hata hivyo, tofauti na ripoti zilizotolewa kwenye
vyombo vya habari vya Malawi, Msemaji Msaidizi wa Polisi wa eneo la Karonga,
George Mlewa alikana ripoti hizo akidai kuwa watu hao nane waliokamatwa
wanachukuliwa kama wahamiaji haramu tu.
“Wakati tunaendelea na uchunguzi wetu kuhusu suala
hili, naweza kusema kuwa ripoti hizo ni uvumi tu,” alisema Mlewa.
Chanzo: The Citizen