POLEPOLE APEWA SHAVU TENA,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey PolePole
ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu
wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi kuchukua nafasi ya Nape Nnauye
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho
kupitia ukurasa wake wa Twitter zinaeleza kuwa kikao chaHalmashauri Kuu ya
Taifa kimemteua Polepole kushika wadhifa huo.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
kimefanyika leo ambapo miongoni mwa mambo mengi yatakayojadiliwa ni pamoja na
tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.