MMILIKI WA MTANDAO WA JAMIIFORUMS NAYE AISOMA NAMBA,SOMA HAPO KUJUA
Mwanzilishi wa tovuti ya JamiiForums, Maxence Melo
amekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam kwa kukataa kutoa taarifa za
watumiaji wa mtandao huo.
Taarifa kutoka kwenye tovuti hiyo zinaeleza kuwa
Melo amenyimwa dhamana hivyo atalazimika kukaa rumande mpaka kesho
atakapofikishwa mahakamani.
Jeshi la Polisi linadai kuwa Melo amekataa kuonyesha
ushirikiano kwa Jeshi hilo ambapo walikuwa wakihitaji majina ya baadhi ya
watumiaji wa mtandao huo.
JamiiForums wameeleza kuwa kiongozi huyo (Maxence)
alikataa kutoa taarifa hizo kwa kile alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni
uvunjwaji wa Sheria na Haki za wananchi.