Meya wa jiji awataka wafanyabiashara wa jengo la Machinga kulipa kodi
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita a kizungumza na wajumbe wa halmashauri ya jiji na menejiment ya soko la kariakoo baada ya kufanya ziara yake Ja
MEYA wa jiji
la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka wafanyabiashara wa jengo la Mchinga
[Machinga Comlex] kulipa kodi ili kuwezesha jiji kulipa deni la sh. Bilioni 41
wanazodaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya jamii [NSSF].
Meya Isaya
ametoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa ziara yake ya kukagua mali za jiji iliyohusisha wajumbe wa
Halmashauri ambapo alifika katika jengo hilo na kuelezwa na Kaimu Meneja kwamba
wafanyabiashara hawalipi kodi kutokana na kile walichokisema kwamba hawatambui
uwepo wake hapo.
Aidha
kutokana na kauli hiyo, Meya alipita kwenye kila kibanda na kuzungumza na
wafanyabiashara ambao wamepanga kwenye vizimba hivyo ambapo wafanyabiashara hao
walimweleza kuwa sio kwamba hawataki kulipa kodi bali wanachotaka ni kupewa
risitizi.
Wafanyabiashara
hao kwa nyakati tofauti walisema kwamba wamekuwa wakilipakodi kwa muda mrefu
lakini hawapewi raisiti jambo ambalo halikubaliki na hivyo kumuomba Meya wa
jiji awapatie risiti ili waweze kulipa kodi wanazodaiwa.
“ Mheshimiwa
Meya wa jiji, sio kwamba hatupendi kulipakodi, tunalipa ila jambo ni moja
wanatupa risiti za mkono, ingawaje kunawengine ambao tunadaiwa miezi kadhaa,
ila wanaodai huja kwa kushtukiza na kutufungia vibanda vyetu,jambo hilo pia
linatukwaza, kama wengine sisi walemavu” alisema mfanyabi.
Meya wa jiji
alitumia nafasi yake kuwaeleza wafanyabiashara kwamba wanatakiwa kulipa kodi
kwa kuwa wanadeni kubwa kutoka NSSF, na kwamba iwapo watashindwa kulipa deni
hilo, jengo hilo litauzwa na hivyo kukosa sehemu ya kufanyia baishara zao.
Aliwaeleza
kwamba hatua iliyopo hivi sasa, ni lazima deni hilo lilipwe bila kujali nani
ambaye alisababisha kuwepo kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha na kwamba kama
watakaidi hali ya wafanyabishara itakuwa ngumu kutokana na kukosa sehemu ya
kwenda.
Alisema
iwapo wataweka utaratibu wakulipa kodi kwenye vibanda ambavyo wanadaiwa,
itasaidia kufidia kulipa deni hilo ambapo hadi kufikia Januari 2017 jiji
litakuwa likidaiwa bilioni 41, hivyo ni vyema wakaweka utaratibu wakulipa kodi
wanazodaiwa.
“ Ndugu
zangu nawaomba sana, mlipe kodi, hili jengo linatusaidia wote, leo hii
likipigwa mnada na kuuzwa akaleta mtu mwingine kumiliki, mnazani mtakwenda
wapi, mnapokataa kulipa kodi.
Aidha aliwaeleza
wafanyabishara hao kwamba, tayari jiji limenunua mashine za kutosha na kwamba kuanzia
Januari mwaka 2017 wanatakiwa kupewa risiti za mashine ya Kilekronikia na
kukataa kupewa ritizi za mkono.
“ Hili suala
la kupewa risiti, kuanzia Januari mtaanza kupewa , msikubali kulipa kodi
bilakupewa risiti za EFDs, mashine zipo za kutosha na kwamba hakuna sababu ya
kupewa mashine za mkono, ila kwa sasa lipeni wakati mkisubiri mashine hizo zije”
alisisitiza Meya Isaya.
Hata hivyo
alisema baada ya ziara hiyo, wajumbe wa kamati hiyo kwa kushirikiana na
washauri wengine watafanya kikao cha tathmini na hivyo kuazimia namna ya
uendeshaji wa jengo hilo ili jiji liweze kupata mapato.
Awali
akisoma taarifa ya jengo hilo, Kaimu Meneja Mkuu wa Machinga Complex alisema kwamba jengo
hilo lina changamoto mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa vizimba vingi ambavyo
havijapata wapagaji.
Alisema
mbali na hivyo,lakini pia hata vizimba ambavyo vinawapangaji bado ni changamoto
kutokana na kukosekana kwa watu kununua bidhaa zilizopo kwenye jengo hilo na
hivyo wengi kuishia kwenye soko la Karume.
Alisema
kutokana na hali hiyo mzunguko wa biashara umekuwa mdogo na hivyo kumuomba Meya
wa jiji na wajumbe wengine kuangalia namna ya kuliwezesha jengo hilo kuingiza
mapato.
Hata hivyo
alisema changamoto nyingine anayo kumbana nayo ni baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam Poul Makonda kuwaeleza wafanyaviashara hao wasilipe kodi kwa kipindi
cha miezi mitatu na kwamba hadi sasa hajafika kutengua kauli hiyo jambo ambalo
lifanya wafanyabiashara kudiriki kusema kwamba hawamtambui uwepo wake.