Zinazobamba

MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAONGEZEKA MARA DUFU,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhb1CGPpbz5vOYRfJdsRUl6-VReNctFkV34cSSZajcKiRMaZ9JoyPfVPNhn_O57SnlUS2H2SenkhIULj9W04x26HmlJNkcrYeSnIVFIyi-JO7NbOiJhdAG3k8IrxGeinv4u5DNTDsU3kywZ/s1600/IMG_20161010_094707.jpg
NA KAROLI VINSENT
MAUZO katika soko la hisa la mkoa wa Dar es Salaam (DSE)yameongezeka mara 6 kutoka milioni 198 kwa wiki iliyopita hadi kufikia Tshs.1.22 Bilioni kwa wiki iliyoishia Desemba 9 ya mwaka huu.
Hata hivyo,Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki iliypita yameongezeka  kwa asilimia 44 kutoka wa hisa 262,589 kwa wiki iliyopita hadi kufikia hisa 378,149 kwa wiki hiyo ilishoishia pia Desemab 9.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa  Mwandamizi wa mauzo  wa  (DSE)Marry Kinabo wakati wa mkutano na waandishi wa habari amesema sababu iliyochangia ongezeko hilo la mauzo imetokana na wawekezaji wengi kwenye soko  kuwekeza zaidi kwenye kununua hisa na sio kuwekeza kwenye hati fungani.

Kinabo amesema ukubwa mtaji wa soko wa makampuni kwa ujumla umeshuka kwa asilimia 0.5 kwa makampuni ya ndani  kwa kuendelea kubaki kiwango kile kile cha trioni 8.
Ameongeza kuwa katika sekta ya viwanda imeshuka kwa point 104.63 na sekta ya huduma za kibenki na fedha imeshuka kwa point 3.66 .
Kinabo amezitaja pia Kampuni tatu zilizoongoza idadi kwa mauzo ni DSE kwa silimia 47,Benki ya DCB kwa silimia 19 pamoja na kiwanda cha TBL kwa silimia 18