LOWASSA ATOA NENO MGOGORO WA CUF,SOMA HAPO KUJUA
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amevunja ukimya kuhusu mgogoro wa uhalali wa
Uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa unaoendelea ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF) ambao umekuwa
ukihusishwa naye tangu awali.
Lowassa
ambaye alitajwa na Profesa Lipumba kuwa chanzo cha yeye kujiuzulu kabla ya
kurejea tena miezi 9 baadae kutengua uamuzi wake, amesema kuwa shida za chama
hicho ni shida za vyama vyote vinavyounda Ukawa.
Mwanasiasa
huyo mkongwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ametumia ukurasa wake wa
Facebook kueleza jinsi ambavyo Ukawa inalibeba tatizo la mgogoro wa CUF.
“CUF
ni wenzetu katika Ukawa. Shida zao ni shida zetu, vita vyao ni vita vyetu,
kushindwa kwao ni kushindwa kwetu, ushindi wao ni ushindi wetu,” aliandika
Lowassa.
Kauli
hiyo ya Lowassa imekuja miezi michache baada viongozi wa Ukawa kueleza msimamo
wao kuwa hawamtambui Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na kwamba
wataendelea kushirikiana na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif
Hamad.
Naye
Profesa Lipumba amekuwa akieleza kuwa hayuko tayari kuona Chadema au Lowassa
wanakinunua chama hicho.
Hivi
karibuni, Ukawa wameweka msimamo wao kuwa watawasimamisha wagombea wa pamoja
katika uchaguzi mdogo utakaofanyika mwakani.
Hata
hivyo, kumekuwa na changamoto baada ya pande mbili zinazovutana ndani ya CUF
kila mmoja kutangaza kuwasimamisha wagombea wake huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi
ikiweka msimamo kuwa ili iwatambue wagombea wa chama hicho ni lazima fomu zao
zisainiwe na pande mbili zinazovutana.
Miezi
michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Profesa Lipumba
alionekana akimtambulisha Lowassa mbele ya waandishi wabari na kujibu maswali
mengi yaliyoelekezwa kwake lakini siku chache baadae alitangaza kujiuzulu akida
moyo wake unamsuta hawezi kumuunga mkono mwanasiasa huyo.