HASIMU RUNGWE AJITOSA KUMPAMBANIA PEDESHEE NDAMA,SOMA HAPO KUJUA
Wakili wa kujitegemea, Hashimu Rungwe amejitokeza
kumtetea mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani Hussein
maarufu kama ‘Pedeshee Ndama mtoto wa Ng’ombe’.
Rungwe aliyekuwa mgombea urais kupitia Chaumma
katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alijitokeza jana na kujitambulisha mahakamani
kuwa ndiye atamtetea mshitakiwa huyo.
Ndama mtoto wa ng’ombe (44) anakabiliwa na mashtaka
ya kughushi, kutakatisha fedha na kujipatia dola za Marekani 540,390 kwa njia
ya udanganyifu.
Baada ya kujitambulisha mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Victoria Nongwa, Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa alisema kesi hiyo
imepangwa kutajwa, upelelezi bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe
nyingine. Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 27,2016.
Mshtakiwa huyo alipelekwa rumande kwa sababu
miongoni mwa mashtaka yanayomkabili limo shtaka la kutakatisha fedha ambalo
halina dhamana.
Katika kesi hiyo, Ndama anadaiwa kuwa Februari
20,2014 jijini Dar es Salaam, alighushi kibali cha kusafirisha madini kuonyesha
kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa
kusafirisha kilo 207 za dhahabu yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000
kwenda Australia wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Machi 6, 2014 jijini
Dar es Salaam alitengeneza kibali cha Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam
akijaribu kuonyesha dhahabu hiyo kutoka Congo inatarajiwa kusafirishwa kwenda
Australia.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na
Machi 2014 katika jiji la Dar es Salaam alitakatisha fedha kwa kufanya muhamala
wa dola za Marekani 540,390 kwa kuelekeza ziwekwe katika akaunti namba
9120000085152 iliyopo katika benki ya Stanbic yenye jina la Muru Platnum
Tanzania Investment Company Limited na kuanza kuzitoa taslimu wakati akijua
fedha hizo zinatokana na zao la uhalifu