Zinazobamba

TUKIO KUBWA ALILOFANYA RC MAKONDA,SOMA HAPO KUJUA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametimiza ahadi zake kwa kwa jamii, taasisi, watendaji na watu binafsi kufuatia ziara yake ya Dar Mpya iliyoanza Novemba 18 mpaka 28 ambapo alikutana na kero mbalimbali zilizohitaji ufumbuzi ili kuondoa changamoto kwa makundi hayo tajwa.rc-makonda-madawati-24

RC Makonda amekabidhi vifaa mbalimbali kwa waliohaidiwa vyenye thamani ya shilingi milioni 164,272,000 ambapo kwa upande wa kituo cha kulea waathirika wa dawa za kulevya kilichopo Kigamboni kinachoitwa  Pedderef House of Wisdom RC Makonda amewapatia jiko la gesi, mitungi miwili ya gesi, king’amuzi, luninga na magodoro 50.rc-makonda-madawati-13

Pia kutokana na utendaji mwema wa watendaji wa mitaa na wenyeviti RC Makonda amemkabidhi Mtendaji wa Kata ya Buyuni pikipiki 1 na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni piki piki 1, huku kwa watumishi wanne ambao utendaji wao umedhihirisha hali yao ya utayari wa kujitolea na kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu ambao amewazadia watumishi kulala katika Hoteli ya Kilimanjaro ambao ni Dr Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mruto Kamanda Polisi Mkoa wa Temeke, Edward Otieno Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Sekretarieti ya Mkoa na Aron Joseph Mkurugenzi wa Uendeshaji DAWASCO.rc-makonda-madawati-24

Kuhusu suala la ujasiriamali RC Makonda amekabidhi Milioni Moja kwa kijana Evans Tulizo wa Soko la Sterio Temeke, pia amempatia kiasi cha shilingi laki mbili mjasiriamali mdogo kwa ajili ya biashara yake ya machungwa, kuhusu changamoto ya maji RC Makonda amemkabidhi Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko cheki ya shilingi milioni 13 ili wananchi wa Gongo la Mboto na Pugu waweze kupata Maji na kuiondoa changamoto iliyokuwa inatokana na ubovu wa miundombinu, huku akiongeza kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni mchango kwa ajili ya kukamilisha ununuzi wa tanki la maji kwa wananchi wa Buyuni na kata ya Pemba Mnazi.rc-makonda-madawati-31

Kwa upande wa kuunga Mkono ujenzi na ukarabati RC Makonda amekabidhi mabati 2000 katika shule ya Sekondari Jitegemee huku shule ya Msingi Mbagala Annex ikikabidhiwa mabati 1000, Shule ya Katoliki ikikabidhiwa mifuko 1000 ya saruji, Matofali 10000 kwa ajili ya kanisa la AIC, Mabati 300 kwa ajili ya Soko la Samaki Msasani, Mabati 200 kwa ajili ya uwanja wa Taifa, Tumba kwa ajili ya kwaya ya JWTZ na gari la kubebea wagonjwa kwa Polisi FFU Ukonga na msaada wa fedha za matibabu wenye jumla ya shilingi milioni nne kwa watu mbalimbali hususani wazee na kina mama.rc-makonda-madawati-27

Huku kwa upande kamanda kanda maalumu ya Dar es salaam Stanley kabiki ametoa shukrani zake kwa RC Makonda baada ya kupatiwa msaada wa gari la kubebea wagonjwa ambalo lilikuwa ni changamoto kubwa kwa upande wao kwa kipindi kirefu kwa wanahudumia wakazi wengi ikiwemo wanaotokea Msongola na Chanika, huku akihaidi watalitumia bila ubaguzi wowote.rc-makonda-madawati-17 rc-makonda-madawati-14 rc-makonda-madawati-9 rc-makonda-madawati-8 rc-makonda-madawati-51

Jiunge