Zinazobamba

DC HAPI AWAANGUKIA MAWAKALA WA MISUTU,SOMA HAPO KUJUA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Salum Hapi amewaomba Wakala wa Misitu nchini (TFS) kumsaidia mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 1068 kwa shule zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondon
Mkuu wa Wilaya ya huyo ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni tano na laki sita kutoka kwa Wakala wa Misitu nchini kanda ya Kinondoni.
DC Hapi ameeleza kuwa wilaya yake imemaliza tatizo la madawati hata waliyoyapokea leo ni ziada tu, hivyo ametumia fursa hiyo kumuomba Meneja wa Wakala wa Misitu Alex Mbaga kuwasaidia mbao kwaajili ya ujenzi wa madarasa kwa kuwakea milango na madirisha kwani tayari wamepokea msaada wa saruji na mabati yav kutosha kwa ajili ya vyumba hivyo mbao hizo zitawasaidia kurahisisha kazi.
Hapi ameongeza kuwa katika kipindi hiki kifupi wameweza kujenga shule mbili ambazo fedha za ujenzi huo zimetokana na mchango wa Rais  Dkt John Pombe Magufuli.