BIFU LA MPAKA KATI YA TANZANIA NA MALAWI LAIBUKA TENA,SOMA HAPO KUJUA
Wengi wakisikia kuna mgogo hapa Tanzania na nchi
nyingine watakuwa wanashangaa sana haswa kutokana na ukweli kwamba nchi hii ni
nchi pekee ambayo haijapitia misukosuko ya mgongano wa uvunjifu wa amani tangu
taifa hili lizaliwe, lakini hata historia inatuambia kuwa tumepata uhuru kwa
amani kabisa bila ya kutumia bunduki mwaka 1961.
MGOGO UMEZUKA TENA
Kama ulikuwa hujui Malawi na Tanzania zilikuwa
katika mgogoro tangu mwaka 1890. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki
wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya
Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande
wa Tanzania.
Mgogoro huo unatoka na ziwa Nyasa ambalo kwa mujibu
wa Tanzania Ziwa hilo limekatwa katikati upande Tanzania upande Malawi, lakini
cha ajabu Malawi wanalitaka lote liwe lao wengi walikuja kujua mgogoro
huu mwaka 2011 wakati Jakaya Kikwete akiwa madarakani jitihada zilifanyika na
zilikoma sasa wameibuka tena.
Malawi wameandika barua umoja wa Afrika kwa lengo la
kutatua mzozo huo ambao unaelekea kuwa mkubwa sasa kumbuka Kwa Tanzania,
ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago
Niassa.
Mwaka 2012 Tanzania ilisema kuwa ingelinda mipaka
yake hivyo kuibua hofu baina yao lakini kwa taifa letu bado liko na amani na
mzozo huu utapatiwa ufumbuzi, lazima wakae chini iliipatikane suluhu iliyokuwa
na mwisho. ‘Credit’ kwa BBC