WABUNGE WAMKOMALIA RAIS MAGUFULI WAMGOMEA SUALA HILI,SOMA HAPO KUJUA
Wabunge wamegomea hatua ya Serikali kutaka
kusimamia posho na marupurupu yao, huku wakitaka suala hilo waendelee
kujipangia wenyewe.
Msimamo huo uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Katiba
na Sheria, umetolewa baada ya Serikali kuwasilishwa Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba tatu ya mwaka 2016.
Awali Serikali ilitaka suala la stahiki hizo kwa
watumishi wa umma liamuliwe na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora.
Akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na
Sheria, Mohammed Mchengerwa, alisema wametoa pendekezo hilo katika Sheria
ya Utumishi wa Umma sura 298 kulinda dhana ya mgawanyo
wa madaraka.
“Tume ya Utumishi wa Bunge na Tume ya
Utumishi wa Mahakama zipewe uhuru kusimamia upangaji wa mishahara, posho
na marupurupu mengine,” alisema.
Akizungumzia mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu,
alisema kifungu cha 18 cha Muswada huo kuhusu muda wa mnufaika
kurejesha mkopo, Mchengerwa alisema kamati inashauri mkopo uwe mwaka mmoja
baada ya kumaliza masomo.
Alisema hali hiyo itasaidia kutoa fursa kwa mnufaika
kuanza kulipa mkopo wake, utaratibu ambao hutumika katika nchi
nyingine kama Kenya na Zambia.
“Kuhusu wanufaika waliojiajiri kamati
inapendekeza kiwango cha kurejesha mkopo kisipungue Sh 100,000 badala ya Sh
120,000 kama Serikali ilivyopendekeza,” alisema Mchengerwa.
Awali, akiwasilisha hotuba ya mabadiliko ya sheria
hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema
kifungu cha 8 cha Sheria hiyo kinaanisha mamlaka ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
(Utumishi) kuwa ni pamoja na kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuendeleza ufanisi
wa utumishi wa umma.
Alisema Ibara 24 ya Muswada huo inapendekeza
kuongeza kifungu kipya cha 9A cha Sheria kinachoweka masharti kuwa Taasisi,
Wakala au Tume za Serikali hazitakuwa na mamlaka ya kuidhinisha mishahara na
marupurupu kwa watumishi wa taasisi hizo na badala yake kibali kwa ajili hiyo
kitatolewa na Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais (Utumishi).
“Marekebisho hayo yanalenga kuwa na
mamlaka moja inayoratibu mishahara, posho na marupurupu na watumishi katika
taasisi za Serikali na pia kuwianisha mishahara posho na marupurupu mengine kwa
watumishi wa taasisi hizo.
“Masharti yaliyopendekezwa hayatatumika.
Ibara hiyo imefutwa na kuandikwa upya masharti yanayopendekezwa hayatatumika
kwa mishahara, marupurupu na masilahi mengine kwa Bunge,Mahakama, Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi,Magereza,JKT, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
na Idara ya Usalama wa Taifa ili utaratibu huo kuendelea kama ilivyo sasa
katika sheria zinazosimamia taasisi hizo.
“Kifungu cha 20 (1) (c) cha Sheria ya
Utumishi wa umma kinaipa Tume ya Utumishi wa Umma mamlaka ya kutunga kanuni
kuhusu usaili wa watumishi wa umma unaofanywa na tume hiyo,”
alisema Masaju
Awali kifungu cha 8 kilikuwa kinapendekeza
kufanyiwa marekebisho kumpa mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi)
kurekebisha na kuwianisha mishahara, posho na marupurupu mengine kwa
watumishi wa umma wakiwamo wabunge na idara ya mahakama.
Huku ikipendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A
kinachozizuia taasisi za umma, wakala, bodi na tume zisirekebishe au kuwianisha
mishahara, posho na marupurupu mengine kwa watumishi.
Sehemu ya tano inapendekeza marekebisho katika
Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 kwa lengo la kutoa tafsiri ya neno
“recruitment secretariat”, maneno hayo yametumika katika Sheria lakini hayakuwa
yamepewa tafsiri.
Kiama kwa waajiri
Alisema Ibara ya 19 ya Muswada huo, inapendekeza
kufuta kifungu cha 20 na 21,ambacho kilikuwa kinaeleza kwa kuwa si rahisi
mwajiri kufahamu kama mtumishi anayeajiriwa ni mnufaika wa mkopo.
Kutokana na hali hiyo,alisema Muswada unaainisha
kuwa mwajiri atatakiwa kuifahamisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 28,baada ya
mwajiriwa huyo mwenye Shahada au Astashahada ili bodi iangalie kama
mwajiriwa huyo ni mnufaika wa mikopo.
“Mwajiri ambaye atashindwa kutekeleza
masharti ya kifungu hicho atakuwa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni
Sh milioni moja au kifungo cha miezi sita gerezani. Pia inapendekezwa baada ya
mnufaika wa mkopo mwajiri atatakiwa kukata asilimia 15 ya mshahara wa
mwajiriwa.
“Bodi au mawakala wake wawe na mamlaka
ya kukagua kumbukumbuku za waajiriwa kwa lengo la kufuta taarifa zinazohusiana
na wanufaika wa mkopo pamoja na kumbukumbu za waajiriwa kwa lengo la
kutafuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo kwa hatua zao muhimu
kuhusu makusanyo wa mikopo,” alisema
AG Masaju alisema kifungu cha 57 cha sheria hiyo,
kinaweka masharti kuhusu zuio kwa shughuli za binadamu zinzoathiri ulinzi wa
bahari, mito, mabwawa zisifanyike ndani ya mita 60 kutoka kingo za bahari, mito
au mabwawa.
Alisema hatua hiyo imekusudiwa kuimarisha ulinzi na
usalama wa mazingira ya maeneo husika ya bahari, maziwa na mito na mabwawa.
“Ibara ya 11 ya Muswada inapendekeza
kifungu hicho kirekebishwe katika kifungu kidogo cha pili kuweka
mwongozo wa namna ya kupima mita 60 ambako shughuli za binadamu zimezuiliwa
kufanyika.
“Kifungu cha 184 kinaeleza athari na
uthamini wa mazingira. Ibara ya 12 inapendekeza kuwa kitendo cha mtu yeyote
kushindwa au kukataa kufanya tathimini ya athari za Mazingira kwa mradi
unaohitaji tathmini hiyo kufanyika ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini
isiyopungua Sh milioni tano na isiyozidi Sh bilioni moja au kifungo
kisichopungua miaka miwili,” alisema.