MANENO ALIYOTAMKA MAREHEMU SAMWELI SITA KABLA HAJAFA,SOMA HAPO KUJUA
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume
ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika
maisha.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya wa
Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa
baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza
kuwa asingeweza kupona.
“That’s life (hayo ndiyo maisha),”
Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya
mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University
of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa
maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele
hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.
Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na
matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi
dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya
kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja
kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha
Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.
Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo
Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo
ndiyo inayoratibu mazishi
“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye
tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale
aliyokuwa akituelekeza,” alisema Benjamini.
Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake
halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!