UTAWALA WA MAGUFULI WAKOSOLEWA VIBAYA,CHAMA CHA NCCR MAGEUZI CHAUVAA UTUMBUAJI WAKE MAJIPU,SOMA HAPO KUJUA
![]() |
Pichani aliyeshika kitabu Chekundu ni miongoni mwa watendaji walioamuliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukamatwa kwa madai ya kuuza viwanja vya wananchi |
Chama
cha Nccr Mageuzi kimeukosoa vikali mwenendo wa utawala wa Rais John
Magufuli hatua yake ya kuwasimasha au kuwafukuza kazi watendaji wa serikali ambayo imebeba jina la
(Utumbuaji majipu),huku chama hicho kikidai hatua hiyo imezidisha uoga kwa watumishi
na kuchangia kuzoletesha uwajibikaji,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli
hiyo ya Nccr mageuzi inakuja ikiwa ni siku moja kupita baada Chama cha
wafanyakazi nchini (TUCTA) kumlalamikia waziri mkuu hatua hiyo kwa kusema
inakwenda kinyume na sheria za kazi na ajira.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katibu mkuu wa Nccr Juju
Banda amesema kitendo cha mawaziri, wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya
kuwafukuza watendaji wa serikali bila hata kufanya uchunguzi kinakwenda kinyume
na sheria za kazi na kuleta uoga kwa watumishi.
Amesema
Chama hicho,hakipingi uchukuaji wa hatua
kwa watu wanaofanya ubadilifu wa mali za umma bali wanapinga hatua ya inayochukiwa sasa watendaji kwa kile alichodai watumishi wengi wamekuwa wakifukuzwa kazi bila
hata uchunguzi kufanyika,
“Leo
hali ya nchi ni mbaya,watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uoga huku
wakimuogopa mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa,kwani wamekuwa wakifika sehemu za
kazi na kuamulu watumishi wa umma kukamatwa au kufukuzwa kazi bila hata ya
uchunguzi kufanyika,na hii hatua imepeleka watumishi wa umma kufanya kazi kwa
uoga na hali hii itapeleka maendelea kuchelewa”amesema Banda.
Hata
hivyo,Banda ametabili uwenda serikali ikaingia kwenye hasara kubwa ya kuwalipa
watumishi hao ambao inawafukuzwa kwa kile alichodai watumishi hao wakiamua
kwenda kwenye vyombo vya mahakama
wakipinga kufukuzwa wao kazi ambapo kumejaa uonevu na kupelea mahakama kutoa
haki ya wafanyakazi hao.
Katika
Hatua nyingine Chama hicho kimetanga kuanza ziara nchi nzima yenye lengo la
kukijenga chama hicho kueleka kwenye chaguzi zinazokuja mbeleni.