RC MAKONDA AIBUKA NI HICHI LEO,SOMA HAPO KUJUA

Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amepiga marufuku wauzaji holela wa
samaki na mboga mitaani badala yake wapeleke katika masoko maalumu.
Aidha
ameliagiza jeshi la polisi na halmashauri zote mkoani humu kuwakamata
wafanyabiashara watakaokiuka agizo hilo.
Makonda
alitoa kauli hiyo jana, wakati alipotembelea Soko la Kimataifa la Samaki la
Feri na kuzungumza na wafanyabiashara wa soko hilo, ikiwa ni sehemu ya ziara
yake ya siku mbili katika Wilaya ya Ilala.
Wafanyabiashara
hao walieleza kuwa, moja ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na kuzagaa kwa
wafanyabiashara huria wa samaki hususani katika vituo vya mabasi ya daladala na
pembezoni mwa barabara mkoani humo.
Walidai
kuwa, hali hiyo inahatarisha uhai wa soko hilo kwani watu wengi hawafiki
kununua samaki katika soko hilo, badala yake huishia kununua katika vituo vya
mabasi na mitaani.
Mfanyabiashara
Said Ally alimueleza mkuu huyo wa mkoa kuwa, masoko huria ya mitaani
yanaendelea kushamiri huku viongozi wa halmashauri na wananchi wakikaa kimya.
“Mkuu
wa mkoa tusaidie sasa hivi kila kona kuna wauza samaki hasa katika vituo vya
mabasi jambo linalosababisha feri tunakosa wateja wanaishia mtaani, soko
litakufa kwa sababu watu hawaji tena tofauti na awali,” alisema Ngasa.
Mbali
na hayo wafanyabiashara hao waliomba kuboreshwa kwa miundombinu ya soko hilo
ambayo imechakaa licha ya soko kuwa la kimtaifa.
Kutokana
na malalamiko hayo, Makonda alipiga marufuku biashara ya samaki na mboga
mitaani na kumuagiza Kamanda wa Operesheni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Lucas Mkondya kuwashughulikia wafanyabiashara wote watakao kiuka agizo hilo
kuanzia sasa.
“Ni
marufuku kufanya biashara ya samaki na mboga katika maeneo ambayo sio rasmi
wafanyabiashara wapeleke katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kufanyia
biashara hizo,” alisema
Makonda.