Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AFUNGUKA SABABU YA KUIVUNJA BODI YA TRA,KUMBE KISA NI HIKI,SOMA HAPO KUJUA

RAIS John Magufuli amefichua sababu ya kuvunja bodi ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) baada ya kudai bodi hiyo iliziweka fedha zaidi ya bilioni 26 kwenye Benk Binafsi na kufungua Akount ya Fixed DepositeAccont.



Akizungumza katika Maafali ya 30 ya chuo kikuu Hulia nchini Rais Magufuli amesema,


"Sasasifahamu kama Chuo Kikuu Huria na nyinyi mmekuwa mkiweka fedha za maendeleokatika Fixed Deposit Account, lakini huo ndio umekuwa ni mchezo, juzi hapatumekuta fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 26 zilizokuwa zimetolewa na Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya matumizi ya TRA, zikapelekwa kwenye benki
tatu kama Fixed Deposit Account na Bodi ya TRA ikapitisha, ndio maana nilipozipata hizo taarifa, fedha nikachukua na Bodi kwa heri.


"Hata kwasasa hivi Waziri upo hapa, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambayo ilianzishwa kwa sababu maalum, inachangiwa fedha wakati kuna fedha zao wameziweka kwenye Fixed Deposit Account, Waziri hiyo ni message sent and Delivered" amesisitiza Rais Magufuli.
Aidha, RaisMagufuli amewaonya viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali ambaowamekuwa wakitumia vibaya fedha za umma ikiwemo kuweka fedha nyingi za Serikalikatika akaunti za muda maalum (Fixed
Deposit Account) kwenye benki za biashara ambako hujipatia fedha kupitia faida ya akiba bila kujali kuwa vitendo hivyo husababisha Serikali kukosa fedha
na kulazimika kukopa kutoka benki za biashara ambako hutozwa riba kubwa.



Katika Mahafalihayo, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amewatunuku shahada na vyeti jumla ya wahitimu 4038, wakiwemo wahitimu 8 wa shahada ya Uzamivu, 217 washahada ya Uzamili, 111 wa Stashahada
ya Uzamili, 1,186 wa Shahada ya Kwanza, 484 wa Stashahada na 1,421 wa vyeti mbalimbali.