SHUHUDIA TUKIO KUBWA LEO KUTOKA KAMPUNI YA WHITEDENT,YAWAPA WASHINDI WAKE MAGARI MAPYAA,SOMA HAPO KUJUA
Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO
ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi HAMISI SAID zawadi ya gari baada
ya kuibuka mshyindi wa Tatu katika Promosheni hiyo
|
24 Novemba 2016. Dar es
Salaam. Kampuni inayoongoza katika bidhaa za afya ya mdomo
Whitedent imekabidhi magari 25 ya aina ya Suzuki Alto K10 kwa washindi kutoka
mikoa mbali mbali nchini walioshiriki promosheni ya miezi mitatu iliyokuwa inasheherekea
kuadhimisha miaka 25 ya biashara hiyo.
Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi Julai mwaka
huu ilitoa nafasi kwa maelfu ya wananchi kushiriki shindano hilo kwa kukisia
idadi ya pakiti za whitedent zilizomo ndani ya moja ya magari hayo ya aina ya
Suzuki yaliyokuwa yakizunguka nchi nzima wakati wa promosheni. Washiriki
walitakiwa kujaza fomu ya ushiriki katika kipindi hicho cha promosheni na
kukisia jibu sahihi ili waweze kuingia katika droo kubwa ya kujishindia moja ya
magari hayo ya Suzuki Alto 10 kabla ya mwisho wa Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
katika hafla ya makabidhiano jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Uendeshaji wa
Chemi & Cotex Raja Swaminathan alisema, “Nina furaha leo
ya kuyakabidhi magari haya kama ishara ya kusheherekea miaka 25 ya mafanikio
pamoja na jamii yetu. Tofauti na mashindano mengine yoyote, kila mshindi
atapokea gari lenye maili sifuri pamoja na kadi yake ya usajili, bima ya
mwaka mmoja, likiwa limejazwa mafuta tenki nzima na gharama zote za kodi
kulipwa. Hii haijawahi kufanyika nchini Tanzania.”
Shindano
hilo lililokuwa chini ya uangalizi mkubwa na wa makini wa Bodi ya Bahati Nasibu
Tanzania lilichukua miezi mitatu na kushirikisha mikoa yote ya Tanzania bara na
visiwani Zanzibar.
"Tulitaka kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika
shindano hili. Bidhaa
ya Whitedent ni ya kujivunia ya Tanzania kwa Watanzania ikiwa imetengenezwa na
Watanzania. Safari ya promosheni ilipita sio mijini tu bali pia katika vijiji
ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kushiriki,” aliongeza Raja
Swaminathan, Afisa Mkuu Uendeshaji wa Chemi & Cotex.
Inakadiriwa
kuwa zaidi ya wana Afrika mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa kupiga
mswaki kwa kutumia Whitedent. Nchini Tanzania kupitia ukaguzi wa Nielsen wa
mwaka 2012 ulionyesha kuwa Whitedent ina asilimia 79 ya soko nchini na
hupatikana katika maduka makubwa ya bidhaa hadi kwenye vioski vidogo.
Whitedent,
inajivunia kuwa na asili ya Tanzania na ni bidhaa inayotengenezwa kwa ubora wa
hali ya juu katika kiwanda chenye vifaa vya kisasa jijini Dar es Salaam.
Vilevile dawa hii ya meno hutengenezwa kwa viwango vya kimataifa.
“Mafanikio makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa
uwezo wa viwanda nchini kwetu ni mkubwa na tuna nafasi kubwa ya kukua na
kutengeneza bidhaa bora kwa Watanzania kwa bei nafuu na pia kuweza kuuza
ulimwenguni kote. Tunajivunia kuwa katika viongozi wa mafanikio
haya,”alimalizia Swaminathan.
Hafla ya makabidhiano ya magari imefanyika leo rasmi
katika mikoa ya Dar es Salaam, Moshi, Mbeya na Mwanza. Miongoni mwa washindi
hao kutoka Dar es Salaam ni Emmanuel Sitta, Hamisi Saidi Shabani, Abdu Idd
Fereshi, na Ramadhan Khamis Ramadhan. Washindi kutoka Mtwara, Arusha, Dodoma,
Iringa na Shinyanga wanatarajia kupata magari yao tarehe 26 Novemba na wale
kutoka Kigoma, Tabora, Morogoro, Musoma na Zanzibar
tarehe 29 Novemba 2016.
PICHA ZAIDI HIZI HAPO