TAARIFA MUHIMU KWA VIJANA WALIOMBA JKT,SERIKALI YAJA NA HILI HAPA,SOMA HAPO KUJUA
Serikali amewaagiza wote waliohitimu kidato cha sita
Mei mwaka huu na ambao hawajajiunga na vyuo vya elimu ya juu, wakaripoti katika
kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Desemba Mosi, mwaka huu.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk
Hussein Mwinyi ametoa agizo hilo mjini Dodoma alipozungumza na waandishi wa
habari katika Ukumbi wa Habari wa Bunge.
Dk Mwinyi alisema Mei na Juni mwaka huu, JKT
iliwafanyia usaili vijana wa kujiunga na JKT kwa kujitolea. Alisema usaili huo
ulifanyika kwa kushirikiana na kamati za ulinzi za wilaya na mikoa.
“Wizara ya Ulinzi na JKT inapenda
kuwatangazia vijana wote waliosailiwa Juni mwaka huu, kujiunga na JKT kwa
kujitolea, waripoti kwenye kambi walizopangiwa ifikapo Desemba Mosi mwaka huu
kwa nauli zao,” amesema Dk Mwinyi.
Dk Mwinyi amesema mafunzo hayo ni ya miezi mitatu
kwa mafunzo yenye utaratibu wa kawaida na miaka miwili kwa wa kujitolea.
Ili kufanikisha hilo, Wizara ilimuagiza Mkuu wa JKT
kufufua kambi ya Makuyuni JKT iwe miongoni mwa kambi kuanzia Desemba mwaka huu.
Aliagiza kambi za Luwa na Milundikwa za mkoani
Rukwa, zirejeshwe kwa shughuli za JKT za kilimo na ufugaji.
Dk Mwinyi alimuagiza Mkuu huyo wa JKT pia kambi ya
Mpwapwa irejeshwe kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya kilimo na ufugaji ndani ya
JKT.