TAARIFA MUHIMU KUHUSU UKWELI WA TAARIFA ZA KIFO CHA RAMADHANI MAPURI,SOMA HAPO KUJUA
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha
taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe.
Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani)
amefariki dunia.
Taarifa Rasmi ya Serikali ni kwamba taarifa hizo ni
za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Kamishna Balozi Mapuri yupo hai
na afya yake iko vizuri.
Mheshimiwa Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambae kwa
sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka
kwa madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya
Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika.
Serikali imesikitishwa na taarifa za uvumi na uzushi
uliosambazwa jana na leo kwenye mitandao ya kijamii, taarifa hizi sio za
kweli na tunawaomba wananchi wazipuuze.
Aidha, Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari
na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa
Serikali.
Imetolewa na :
Dk. Juma Mohammed Salum
Kny Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO
Zanziba