SERIKALI YA MAGUFULI YAWAREJESHA KAZINI ILIOWATUMBUA MAJIPU,SASA KULIPWA FEDHA ZAO ZOTE,SOMA HAPO KUJUA
Watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) waliosimamishwa kazi baada ya kusafiri nje ya
nchi kinyume na agizo la Rais John Magufuli, wamerejeshwa kazini baada ya
takriban mwaka mmoja kupita.
Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba aliwataja
watumishi hao kuwa ni Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Mary Mosha na Mkurugenzi wa
Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Ekwabi Mujungu ambao wamerejeshwa
baada ya shauri lao kusikilizwa na ofisi husika.
“Shauri lao lilishughulikiwa na Ofisi ya Rais
kutokana na vyeo vyao, wamerejeshwa ofisini na kuanza kazi Novemba 14,”
alisema.
Misalaba alisema watumishi wengine waliorejeshwa
kazini ni aliyekuwa Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani na Katibu Muhtasi wa
mkurugenzi mkuu, Rukia Nikitas shauri lao lilisikilizwa na mamlaka ya taasisi
hiyo na hatua za kinidhamu zilichukuliwa ikiwamo kuhamishwa vitengo.
Watumishi hao walidaiwa kuondoka nchini Novemba 23
mwaka jana, kabla ya kupewa majibu ya vibali walivyoomba baada ya kuandika
barua Ikulu kuhusu safari hiyo.
Rais Magufuli alitangaza kufuta safari za nje ya
nchi kwa maofisa wa Serikali Novemba 7, 2015 na kutoa mwongozo kwamba safari
zitakazoruhusiwa ni zile zenye ruhusa ya Ikulu.
Kusimamishwa kwao kazi kulitangazwa na aliyekuwa
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipozungumza na waandishi wa habari
Desemba 16 mwaka jana.
Takukuru iliiandikia Ikulu barua ya kuomba kibali
kwa ajili ya safari hiyo, lakini kabla ya kujibiwa, wafanyakazi hao waliamua
kusafiri.