AJARI MBAYA YA NDEGE YATOKEA LEO,SOMA HAPO KUJUA
Ndege
iliyobeba watu 81 wakiwemo wachezaji wa klabu ya soka ya Chapecoense kutoka
Brazil imeanguka wakati ikikaribia kutua katika mji wa Medellin nchini
Colombia, mamlaka zathibitisha.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa watu 76 wamefariki dunia huku watano
wakipona.
Maofisa
wa uwanja wa ndege wa Medellin wamesema wachezaji wa Chapecoense waliokuwa
kwenye ndege hiyo walikuwa safarini kwenda kucheza fainali ya Copa Sudemericana
dhidi ya Atletico Nacional ya Medellin, Colombia.
Kutokana
na ajali hiyo, mechi baina ya timu hizo iliyokuwa ichezwe kesho imeahirishwa
hadi itakapotangazwa tena.