CHADEMA YAJA NA MKAKATI WA MPYAA WA KIMAMBANO KUELEKEA 2019 NA 2020,SOMA HAPO KUJUA
Baada
ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina
la ‘Kata Funua’.
Operesheni
hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa
chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.
Mbowe
amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi
mkoani Mtwara.
“Kiongozi
yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili
tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.
Amesema
ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi
hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo
msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.
“Ili
kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote
atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka
kutokea kwa migogoro,” amesema.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli
kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa
majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.
“Safari
hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea
katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye
uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.