WAKATI MBUNGE LEMA AKISOTA RUMANDE,WAPIGA KURA WAKE WAIBUKA NA HIKI MAHAKAMANI,SOMA HAPO KUJUA
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo
amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambapo alirejeshwa rumande
kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri kuhusu rufaa yake iliyokuwa
imekatwa.
Mahakama iliwataka Mawakili wa Lema kuwasilisha
notisi ya rufaa na si rufaa.
Kwa upande mwingine baada ya wafuasi wa mbunge huyo
wamejitokeza mahakamani wakiwa wamevalia fulana zenye maandishi ‘Justice 4
Lema’ ikiwa ni njia ya kuishinikiza mahakama kumuachia mbunge huyo kwa wao
wanaoa kuwa haki haitendeki.
Kesi la Mbunge Godbless Lema imehirishwa hadi
Disemba 2 mwaka huu.