SAKATA LA KATIBA MPYA: JUKWAA LA KATIBA WAMNG'ANG'ANIA RAIS MAGUFULI, WASEMA KAMA YEYE HAJASEMA LAKINI CHAMA CHAKE KIMESEMA
Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) Rais Magufuli hawezi kukwepa kuhusu suala la kupatikana kwa katiba mpya kwani yeye si Rais wa mgombea huru bali amepelekwa na chama ambacho kimewaahidi watanzania kuwa katiba mpya ni miongoni mwa sera zao
Kauli hiyo ya jukwaa la
katiba imekuja huku kukiwa na sintofaamu kuhusu kupatikana ama kutokupatikana
kwa katiba mpya mchakato ambao ulisimama na kupisha uchaguzi mkuu mwaka 2015 na
kuacha katika hatua ya Katiba Pendekezwa.
Akizungumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la katiba Tanzania Ndugu
Hebron Mwakagenda alisema wameshtushwa na kauli ya serikali ya Tano kuwa
mchakato wa Katiba mpya sio kipaumbele cha serikali ilihali katika Ilani ya
chama cha mapinduzi ndio Ilikuwa moja ya ahadi zao za kuhakikisha kuwa katiba
hiyo inapatikana.
Mratibu wa JUKATA Ndugu Hebroni Mwakagenda akizungumza na wanahabari leo. |