DC HAPI AIBUA MADUDU KINONDONI,NI YALE YA TASAF ,AMTUMBUA KIGOGO,SOMA HAPO KUJUA
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi
wa manispaa hiyo,Aron Kagurumjuli kumvua nyazifa za uongoni mratibu wa Mfuko wa
Kusaidia kaya masikini(TASAF) katika wilaya kinondoni Onesmo Oyango baada ya
kubainika kuwaingiza kwenye malipo watu 1,397
ambao hawana sifa ya kuwalipwa fedha za
hizo ambao wameghalimu zaidi ya milioni 266.9.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Hata hivyo,Hapi amewaomba viongozi wa Mfuko huo, ngazi
ya taifa kumchukulia hatua pia mlipaji mkuu wa Taifa kwa hatua yake ya kuhusika
kuwalipa watu hao, huku akijua hawana sifa ya kulipwa stahiki hizo.
Pamoja na hayo,Hapi pia ameiagiza Taasisi ya kuzuia na
kupamba na Rushwa (TAKUKURU) katika
wilaya yake kufanya uchunguzi wa kina kwa wanufaika wote na TASAF ili
kujilizisha kama wsanafuaika hao wanasifa
za kupewa fedha hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
salaam Hapi amesema baada ya uchunguzi
wa kina uliofanywa kwa wanufaika wote wa
fedha hizo ambao walitakiwa kunufaika ni watu masikini ambao hawana hata uwezo
kuhudumia familia zao lakini wameshangazwa na hatua ya kulipwa watu wasiokuwa
na sifa hizo
,
,
“Wamelipwa watu wenye uwezo sio masikini au kaya masikini ambazo zilitakiwa
kusaidiwa na mfuko huu “amesema Hapi.
Ameeleza kuwa mbali na watu hao wasikuwa na sifa pia
wamebaini hata watu walionufaika na fedha hizo hawajulikana hata makazi
wanapoishi jambo analodai limetia shaka ata fedha hizo, uwenda zilikuwa
zinakwenda kwa wajanja wachache.
“Lazima
tumsadia Rais Joh Magufuli kupambana watu wote wanaofanya ufisadi kwa watendaji
,kwahiyo hapa naitaka (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina ,pamoja na taasisi
za kinidhamu kwa wafanyakazi kwa watendaji hawa ili hatua zichukuliwe kwa wate
waliohusika na kadhia hii”ameongeza Hapi