MAUZO KATIKA SOKO LA HISA YAPOROMOKA VIBAYA,SOMA HAPO KUJUA
WAKATI serikali ya awamu ya tano ikisema hali ya
uchumi nchini kwa kipindi cha miezi
mitatu imekuwa kwa asilimia 7.6, Mambo ni kama tofauti katika soko la hisa la Dar es
Salaam (DSE)baada ya mauzo katika soko hilo, kushuka kwa asilimia 87%
kwa kufikia Tzs o.5 Bilioni toka Bilioni
4 kwa wiki iliyopita.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hata hivyo,pia mtaji wa mauzo katika soko hilo umeshuka kwa aslimia 2.5% hadi kufikia trioni 20.4 toka 20.9 kwa wiki iliyopita.
Hayo yameelezwa na leo Jijini Dar es Salaam na Afisa
Masoko Mwandamizi wa (DSE)Marry Kinabo (pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari
ambapo amesema kilichochangia kushuka kwa mauzo hayo kumetokana na mauzo ya hati katika soko hilo, ambapo
amedai wawekazaji wengi wameamua kuwekeza katika kununua hati fungani
kuriko kwenye soko la hisa.
“Wawekezaji wengi wameamua kuwekeza kwenye ununuzi
wa hati fungani na kuacha kuwekeza kwenye ununuzi wa soko la hisa na hili
limechangia kushuka kwa mauzo katika soko,”amesema Kinabo.
Kinabo amefafanua sababu ya iliyowapelekea
wawekezaji hao kuwekeza kwenye hati fungani kumetokana na wawekezaji huo
kulinda mitaji yao, isishuke jambo lilowafanya kuwekeza kukimbilia kwenye
ununuzi wa hati fungani.
Hata hivyo, Kinabo amesema Hati fungani nne zimeuzwa
na kununuliwa kwneye soko hilo na kufikia thamani ya 22.1 bilioni ambalo ni
ongezeko la asilimia 33% ya thamani ya mauzo katika soko la hati fungani kutoka
mauzo ya wiki iliyopita ambapo hati fungani sita ziliuzwa na kunuliwa kwa
thamani ya 16.6 bilioni.
Sanjari na hayo,Kinabo amesema ukubwa mtaji wa makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha trion 8.1
trion sawa na wiki iliyopota.
Pia ametaja viasharia vya sekta ya huduma za
kibenki amesema zimeshuka kwa point 0.52
na kupungua kwa bei ya hisa za DSE kwa asilimia 1.59%