Zinazobamba

HALMASHAURI YA JIJI YA DAR YAWA MBOGO KWA KAMPUNIZI ZA KITAPELI,NAIBU MEYA WA UKAWA ASEMA HAYA SOMA HAPO KUJUA



Dar es Salaam

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesema haitomfumbia macho mtu, kampuni, wazabuni na makandarasi watakaolitia hasara jiji hilo hususani kampuni zilizopewa tenda za ukusanyaji mapato.

Pia imesema haitatoa tenda za zabuni kwa kampuni zisizokuwa na vigezo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Meya wa Jiji hilo, Mussa Kafana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wa kampuni tatu zilizoshinda zabuni za ukusanyaji kodi za maegesho katika halmashauri za manispaa zilizomo katika jiji hilo.

Amezitaja kampuni zilizoshinda zabuni hizo kuwa ni, Kenya Airport Parking Services katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Manispaa ya Kinondoni ilishinda Ubapa, wakati Temeke ikishinda kampuni ya Upauka.

“Tumechaguliwa na wananchi ili kuwaletea maendeleo ambayo yanatokana na mapato yanayokusanywa, hatotafumbia macho mtu yeyote atakayesababisha hasara au kuruhusu mianya ya upotevu wa mapato,” amesema.

Aidha, Kafana amefafanua utendaji kazi wa kampuni hizo baada ya kuwepo kwa malalamiko kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala haina mzabuni wa kukusanya mapato ya maegesho kutokana kwamba aliyeshinda tenda hiyo ambayo ni Kenya Airport Parking Services haijaanza kazi rasmi ya ukusanyaji kodi na kwamba huenda manispaa hiyo ikapoteza mapato.

“Kampuni hizi tatu zilikidhi vigezo, ambapo ya Kenya iliahidi kukuanya Bilioni 54 kwa mwaka na kwamba inatakiwa kukusanya milioni 20 kwa siku, ilitakiwa baada ya siku 28 ilete dhamana ya kazi ya asilimia 10 ya fedha ilizoahidi kutoa kwa mwaka ambayo sawa na bilioni 5.4, lakini hadi sasa haijatekeleza hilo na ndiyo sababu ya kutoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.

Kafana amewatoa hofu wananchi juu ya hilo kwa kusema kuwa kampuni iliyomaliza muda wake imeombwa kuendelea kukusanya kodi za maegesho hadi pale halmashauri itakapotafuta mzabuni mwingine.

Kuhusu utendaji kazi wa kampuni nyingine zilizoshinda zabuni hiyo Temeke na Kinondoni, amesema zimeshaanza kufanya kazi.