CHADEMA YASEMA HAITOKUBALI 2020,SOMA HAPO KUJUA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa
namna yoyote katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza
kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,
“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia
haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la
utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya
pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme
kokote kule”alisema Mashinji.
Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji
amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio
amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza mapambano na rushwa
aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.
Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka
mmoja wa Rais Magufuli, amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga
marufuku mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile
alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.