WAZANZIBAR SASA WAANZA KUKINUKISHA,WATINGA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUUPINGA MUUNGANO,SOMA HAPO KUJUA
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeingia kwenye
jaribio jingine, baada ya Wazanzibari 40,000 kufungua kesi mahakamani kupinga
uhalali wake.
Kesi hiyo ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Haki
ya Afrika Mashariki (EACJ) na Rashid Salum Adiy kwa niaba ya wenzake 39,999,
katika Masijala ndogo ya mahakama hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam.
Wadaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Adiy anasema kuwa msingi wa kesi hiyo ni kwamba
Muungano huo haukuanzishwa kisheria.
“Sisi tunadai Muungano huu hauko kwa
misingi ya kisheria na kutokana na ushahidi tulionao, uko kisiasa tu na jambo
hili linahitaji mfumo na mwenendo wa kisheria kwa kuwa wenye mamlaka ya nchi ni
wananchi,” alisema Adiy.
Alisema kutokana na nyaraka walizonazo wanapinga
hati ya Muungano inayodaiwa ilisainiwa Aprili 22, 1964 na wanapinga uamuzi wa
Baraza la Mapinduzi kuridhia Muungano huo.
Wanapinga barua ya Mei 6, 1964, iliyopelekwa kwa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), kuelezea kutambuliwa kwa Muungano
huo.
Pia, wanapinga uhalali wa barua ya Novemba 2, 1964
iliyopelekwa UN ikielezea matumizi ya jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Sheria iliyopitishwa na Bunge Desemba 10, 1964 ikielezea matumizi ya jina la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Adiy na wenzake wanadai kwa kuwa Muungano ni wa
kisiasa, ndiyo maana hauwezi kuleta manufaa kwa pande zote mbili hususani
uwiano wa kiuchumi na kielimu.
Baada ya kuwasilisha nyaraka zao wanasubiri kesi
hiyo isajiliwe kwa kupewa namba katika Mahakama hiyo na kupangiwa taratibu za
usikilizwaji wake.
Mbali na Wazanzibari 40,000, pia alisema wanayo
majina mengine ambayo watayawasilisha mahakamani baadaye, kesi itakapokuwa
imeanza