BALAA LILOMKUTA FREEMAN MBOWE,SASA KUMKUTA SUMAYE,SERIKALI YAJIPANGA KUMCHUKULIA MALI ZAKE,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
WAKATI ikiwa imepita mwezi mmoja baada ya serikali
kupitia shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kuiondosha kwenye jengo la shirika hilo,
kampuni ya Freemedia ambayo inamilikiwa na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kwa
madai ya kudaiwa Bilioni 1.6 ambapo mali zake zikiwa zinatakiwa kuuzwa kwa mnada
kufidia deni hilo.
Sasa “Songombingo”
kama hilo linaanza kumyemelea Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya
tatu,Fredrick Sumaye,ambapo sasa serikali kupitia kwa afisa Ardhi wa manispaa
ya Kinondoni kumwandia hati ya barua ya siku 90 ya kumtaka ajieleze kwanini ameshindwa
kuliendeleza Shamba lake lilioko Bunju ndani ya manispaa hiyo kabla
hajanyang’anywa eneo hilo na serikali.
Waziri wa Nyumba na Maendeleo na Makazi,William
Lukuvi amewasibitishia waaandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuwa
teyari Manispaa ya Kinondoni imeshamwandikia hati ya barua ya siku 90 ya kujieleza kwa
Sumaye ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Chadema.
“Ninachowaambia katika suala la Ardhi hatuangalii
kama wewe ni mkubwa au mdogo,kama umeshindwa kuliendeleza eneo tunakunyang’anya,kuhusu
huyu Sumaye tumemwandikia hati ya barua ya siku 90 na kumtaka ajieleze kwanini
ameshindwa kuliendeleza kwa mda mrefu,na kama akishindwa kutoa maelezo ya
kueleweka basi tutamnyang’anya kwa kumfutia hati ya kumiliki shamba
hilo”amesema Lukuvi.
Kauli hiyo ya Lukuvi inakuja ikiwa ni teyari Sumaye ambaye
ni Waziri mkuu peke aliyedumu katika kipindi cha miaka 10 madarakani kuriko
mawaziri wakuu wote kuwai tokea nchini,ambapo inaeleza Sumaye aliwai
kulalamika kupitia vyombo vya habari
kuwa serikali inataka kumpora ardhi yake kwa kile alichokiita kisa “yeye yupo
vyama vya Upinzani”
Maamuzi hayo ya Lukuvi yanakuja sambamba ikiwa ndani ya shamba
hilo la Sumaye kuibuka mgogoro
mkubwa kati yake na wananchi waliovamia shamba lake kwa kile wananchi hao wanachokisema
“shamba hilo halijendelezwa “ ndio maana wamelivamia.
Akizungumzia hali hiyo, Kigogo mmoja aliyokoa ndani ya
serikali ya Magufuli ambaye aliomba jina lake lisijitajwe mtandaoni ,amesema
hatua hiyo ya serikali ipo kisiasa tu.
“Tatizo hii nchi inakuwa masikini kutokana na siasa tu ndugu ,hivi ni watu wangapi wapo
ndani ya CCM wanamiliki mashamba makubwa tena hawajaendeleza hawanyang’anywi,leo
ndio wanamuona sumaye tu,hapa wanataka kumkomoa tu”
“Kwanza Sumaye anavielezo tosha kuwa pale anataka
kujenga Chuo kikuu na amechelewesha kwa sababu ya kuweka mipango kamili,lakini
siasa za majitaka za Taifa hili wanakata kumkomoa tu,hapo Sumaye akapambane nao
mahakamani tu haki yake ataipata tu”amesema Mtoa taarifa huyo.