UGUMU WA MAISHA,UKOSEFU WA AJIRA,HALI MBAYA KWA WATUMISHI WA UMMA,NI MASUALA YALIYOMUIBUA LOWASSA,AFUNGUKA NA KUSEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA
Tarehe Kama ya leo mwaka Jana, ilikuwa siku muhimu
sana kwa watanzania na Mimi binafsi.Niliwaongoza watanzania kupiga kura nikiwa
mgombea wa upinzani.
Naamini nilileta sura na msisimko mpya katika siasa
za Tanzania.Nilishirikiana na wenzangu kuionesha nchi yetu Demokrasia maana
yake ni nini.
Napogeuka nyuma kuingalia siku ile, nasikia faraja
kubwa sana hasa kwa jinsi watanzania walivyotuunga mkono na kuonyesha matumaini
makubwa kwetu.Ujasiri na ushapavu wa hali ya juu aliyouonesha Mke wangu Regina
wakati wa kampeni,ulinipa nguvu kubwa.
Chini ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe,tuliendesha
kampeni za kiungwana kama tulivyoahidi.Upepo ule ulivuma kwa kasi mpaka
visiwani ambako Maalim Seif aliporwa dhahiri ushindi.
Kwa mujibu wa Tume isiyo huru ya uchaguzi,
tulishindwa uchaguzi ule.Hatutaki kuendelea kuyalilia maziwa yaliyokwisha
mwagika ambayo hayazoleki, lakini kile ambacho tulikisema wakati ule kwanini
tunataka mabadiliko,hivi sasa kila mtu anakiona.
Pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo
lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri
kulipuka,Elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa,utumishi wa umma umekuwa
kaa la moto,.Nasononeka sana nikiona viongozi wanavyoshindana kuwasweka ndani
madiwani na viongozi wengine wa kuchaguliwa hasa wa UKAWA.
Nawashukuru sana wananchi kwa imani kubwa
waliyoionesha kwangu na UKAWA kwa ujumla.Kumalizika kwa uchaguzi ndiyo mwanzo
wa uchaguzi mwengine, kwahiyo mapambano ndiyo kwanza yameanza.Kasi,nguvu, ari
na hamasa niliyonayo ni kubwa zaidi kuliko wakati mwengine wowote.