WAISLAM NCHINI WAHASWA KUPINGA UKANDAMIZAJI,SHEIKH ABDI ATOA NASAHA NZITO,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni
Naibu kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasharia
Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akizngumza na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam
|
NA KAROLI VINSENT
WAISLAM nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele
katika kupinga vitendo vyote vya dhuruma na ukandamizaji wanavyofanyiwa raia, ili
kujiwekea mazingira mazuri ya baadae.
Hata hivyo,Waislam pia wametakiwa kufanya mambo ya
kumpendeza Mungu katika jamii inayowazunguka ili kuhakikisha wanawasaidi
watu wasiojiweza.
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Naibu
kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasharia Tanzania Sheikh Muhammad Abdi
alipokuwa anazungumza na wanahabari kuhusu kuukaribisha mwaka mpya wa kiislam
mwaka ambao ni wa 1438H katika kalenda ya kiislam pamoja na kumbukumbu ya Imam
Hussein mkutano ambao umefanyika katika msikiti wao uliopo Kigogo Post Jijini
Dar es salaam.
Amesema Waislam wanatakiwa kuongana na kupinga
vitendo vya ukandamizaji na dhuruma vinavyotokea kwa jamii kama alivyofanya Imman
Hussein ambaye alijitolea maisha yake kupinga vitendo vya ukandamizaji
waliofanyiwa wananchi wa afrika ya kati.
“Tunapaswa kumkumbuka Imman Hussein kwa miongoni mwa waislam
waliokuwa mstari wa mbele kupinga dhuruma,kwani yeye hakupigania ubinadamu wa
eneo ,linalomzunguka bali alihakikisha anapigania ubinadamu wa Dunia
nzima,jambo hili linatakiwa kuigwa na waislam wote”amesema Sheikh Abdi.
Sheik Abdi ameongeza kuzungumza kwa uchungu,amesema Imam
Hussein ambaye wanamkumbuka leo ni moja kati ya viongozi wa dini ambao
aliwafunza watu namna ya kupinga ukandamizaji,dhuluma katika jamii pamoja na
kutetea haki za wanyonge hivyo ni wakati wa wananchi wa Tanzania kuanza kufwata
maneno yake na kuhakikisha kuwa wanaenzi yale mema aliyoyaacha katika jamii.
Kiongozi huyo wa kiroho amesema kuwa leo hii dunia inalazimika kuitika wito wa Imam Hussein
ili kuinusuru dunia iliyotapakaa damu kila kona,ambapo akitolea mfano wa
mashariki ya kati ambapo imekuwa ikishughudiwa watoto wanavyochinjwa na maelfu
kukimbia makazi yao kwa sababu ya uharibifu,
Huku pia
katika bara la Africa ikishughudiwa makundi ya kiigaidi yakiibuka katika nchi
nyingi ambapo yamekuwa yakileta madhara makubwa kwa wananchi wasio na hatia
huku akisema kuwa mambo haya ni mambo ambayo yalikuwa yanamkera sana Imam
Hussein na kama angekuwepo angejitokeza kupambana nayo