Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akionyesha baadhi ya
dawa bandia zilizokamatwa baada ya ukaguzi maalum uliofanyika maeneo ya Kanda
ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakati alipoongea na waandishi wa habari katika
mkutano wa kutoa matokeo ya ukaguzi wa dawa bandia huo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo katikati akiongea na waandishi wa habari
hawapo pichani wakati wa mkutano wa kutoa matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa
bandia uliofanyika maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini , wa kwanza
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa na bidhaa Nyongeza Bw. Adonis Bitegeko na
kushoto ni Msajili wa Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe
DAWA
bandia na yasiyo sahihi kwa matumizi ya binadamu yamekamatwa maeneo ya Kanda ya
Ziwa na Nyanda za Juu Kusini baada ya kufanyika ukaguzi maalum wa kutafuta dawa
bandia katika maeneo hayo iliyofanyika hivi karibuni.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti
Sillo wakati wa kutoa Matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa uliofanyika katika
mikoa ya Kanda za Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.
“Kutokana
na ukaguzi maalum tulioufanya katika Kanda za Ziwa pamoja na Nyanda za Juu
Kusini wa kutafuta dawa bandia na zisizo sahihi kwa matumizi ya binadamu
tumefanikiwa kukamata dawa bandia za aina tano ambazo zipo kwenye makundi
mawili ya Dawa za malaria na Viua vijasumu(Antibiotics)” alisema Bw. Sillo.
Aidha
Bw. Sillo amesema kuwa ukaguzi huo maalum umeweza kusaidia kukamata dawa ya
malaria aina ya vidonge vya Quinine ambayo inadaiwa kutengenezwa katika kiwanda
cha Elys Chemical nchini Kenya na nyingine zinatengenezwa hapa nchini
katika kiwanda cha Shelys Phamaceuticals Ltd.
Mbali
na hayo Bw. Sillo amesema kuwa pamoja na kukamata dawa bandia pia zoezi hilo
lilifanikiwa kubaini na kukamata dawa zilizoisha muda wa matumizi ,
zisizosajiliwa na zenye ubora duni zenye thamani ya Tsh. Milioni 17.463.
Bw.
Sillo ameongeza kuwa Ukaguzi huo ulitokana na kuwa na taarifa za awali ambazo
zilionyesha uwepo wa dawa bandia katika maeneo ya Geita na Mara mwezi Agosti na
Septemba mwaka huu na kusistiza kwamba zoezi hilo la ukaguzi linaendelea
nchini kote na watakaokutwa na hatia watachukuliwa hatua stahiki.
Kwa
upande wa Msajili wa Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe amesema
kuwa wataalamu wa madawa watakaokutwa na hatia ya kusambaza na kuhudumia dawa
bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya
dawa , chakula na vipodozi.
“Wataalamu
wa dawa ambao wanasambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha
kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi pindi
watapogundulika” alisema Bi. Shekalaghe.
Zoezi
hilo la Ukaguzi maalum wa dawa bandia ulianza Oktoba 4 mwaka huu linafanywa kwa
ushirikiano wa TFDA, Jeshi la polisi pamoja na Maafisa kutoka Baraza la Famasi
litakuwa endelevu ili kuhakikisha dawa bandia zinatoweka nchini.
TFDA YAKAMATA DAWA "FEKI HIZI HAPA" SOMA HAPO KUJUA
Reviewed by Unknown
on
19:38:00
Rating: 5