CCM YAENDELEA KUMSUMBUKIA LOWASSA NA ZITTO KABWE,SOMA HAPO KUJUA
Ikiwa imepita siku mbili tangu aliyekuwa mgombea wa
kiti cha Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa
mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kueleza tathimni ya utendaji kazi wa serikali
ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli, ambapo alidai kuwa, katika kipindi
cha mwaka mmoja wa uongozi huo, kumekuwepo na ukiukwaji wa misingi ya demokrasia
na utumishi wa umma kuwa kaa la moto.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevunja ukimya na kumjibu kwa kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita alikuwa wa kwanza kukiuka misingi ya demokrasia. Kuhusu utumishi wa umma kuwa kaa la moto, imemjibu kuwa wanao lalamika hivyo ni wale wanaotumiwa kuficha mafisadi na wakwepa kodi.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimevunja ukimya na kumjibu kwa kusema kuwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita alikuwa wa kwanza kukiuka misingi ya demokrasia. Kuhusu utumishi wa umma kuwa kaa la moto, imemjibu kuwa wanao lalamika hivyo ni wale wanaotumiwa kuficha mafisadi na wakwepa kodi.
Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amewaambia waandishi wa habari kuwa Lowassa hastahili kuituhumu serikali ya Rais Magufuli kuwa inakiuka misingi ya demokrasia.
“Demokrasia ya kweli lazima ianze ndani ya chama, ni demokrasia ipi iliyotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima wanachama wao haki ya kuomba kupeperusha bendera za vyama walivyoviasisi, kuvitetea kuvigharamia kwa kuamua kumteua mgombea mtunguo ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania?,” amehoji.
Ole Sendeka ameongeza kuwa “Kitendo hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kulidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya demokrasia.”
Amesema CCM haigopeshwi na matamko ya Lowassa anayotoa katika vyombo vya habari kwa kuwa havitaiathiri na kwamba imemamua kumjibu kwa madai kuwa anapotosha umma kwa kueleza mambo yasiyo na ukweli.
Ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutochukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko.
“Wanasayansi wa masuala ya siasa waiangalie demokrasia ya CHADEMA na UKAWA inavyofanya kazi maana ni kihoja, watuambie njia iliyotumika kuwapata wabunge viti maalumu. Kila kiongozi aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA,” amesema.
Pia Sendeka amemtaka kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kutoichukia serikali ya Rais Magufuli kwa kuwa inatekeleza yale aliyokuwa anayapigania.
“Chuki ya Zitto ya kuendelea kunyooshea kidole serikali ya CCM haina tija, sababu inatekeleza yote aliyokuwa akiyapigania,” amesema.
Katika hatua nyingine, Sendeka amedai kuwa CCM haijashiriki kukihujumu chama cha Wananchi (CUF) kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa kinawachonganisha viongozi wa chama hicho ili kigawanyike.
“Hatuna haja ya kuhangaika na CUF na wapanga siasa za uongozi CHADEMA, hatujashiriki kukivuruga na hatuna muda huo,” amesema.
=======
Ndugu wanahabari,
Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taairifa
za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya
vyombo vya habari zinazolenga kukejeri, kudhihaki, kukatisha tama, kubeza na
kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Seikali zake katika
kuleta maendeleo kwa Watanzania
Kumekuwepo na makala zinazoandikwa na magazeti
mawili ya nje ambazo hutolewa kila baada ya miezi miwili na ambazo zinapotosha
na kuandika habari zisizo za kweli kuhusu Tanzania
Pia, yapo magazeti mawili ya ndani ambayo yamekuwa
yakitoa makala mfululizo kwa kila wiki zinazolenga kumchafua Mheshimiwa Rais na
kuichafua taswira ya nchi yetu.
Tumesikitishwa na waandishi wa makala hizo walioamua
kujivua uzalendo na kushiriki mpango wa kuiharibu heshima na taswira ya nchi
yetu kwa maslahi ya maadui zetu wa nje na baadhi ya wanasiasa. Tunafuatilia
kujua nini kinawasukuma kufanya hivyo na kwa maslahi ya nani ilhali sote ni
watanzania. Je ni tama ya madaraka tu au mengine?. Hakuna anayepinga ukosoaji
bali unapaswa uwe ukosoaji wenye nia njema
Ndugu wanahabari,
Mtakumbuka hivi karibuni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu
aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufisadi ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA,
Edward Lowassa, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari aliyoiita tathimini ya
mwaka mmoja baada ya uchaguzi mkuu wa octoba 25,2015
Katika taairifa yake, alidai kuwa alileta msisimko
mpya katika siasa za Tanzania, kwamba ameshirikiana na wenzake kuionyesha nchi
yetu maana ya demokrasia na kukosoa juhudi za serikali na wateule wa Rais.
Demokrasia kimsingi ni dhana inayohusisha ushiriki
na kuheshimu mawazo ya wengi katika kufikia uamuzi. Ikiwa maana halisi ni hii,
tunajiuliza ni ipi demokrasia aliyoionyesha Lowassa ambayo leo anajisifu kuwa
nayo?
- Tulishuhudia akiwa mgombea Urais wa chama ambacho
hakijui, hakushiriki kukijenga wala kutoa mchango wowote unaompa hadhi ya
kupeperusha bendela huku katiba na kanuni ya chama hicho ikivunjwa.
Kidemokrasia anayepewa fursa ya kupeperusha bendela ya chama chochote makini
duniani ni kiongozi au mwanachama aliyethibitika kwa imani na matendo,
kuzielewa, kuzitekeleza, kuzitetea falsafa, itikadi na malengo ya msingi ya
chamahicho. Mgombea ni taswira halisi na alama muhimu inayoakisi dhamira ya
chama husika machoni kwa wananchi.
- Demokrasia ya kweli lazima ianzie ndani ya chama,
ni demokrasia ipi inayotoa mamlaka kwa vyama vinavyounda UKAWA kuwanyima
wanachama wao haki ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera za vyama
walivyoviasisi, kuvitetea, kuvigharamia na walivyovitumikia kwa kuamua kumteua
mgombea “MTUNGUO” (ambaye hajapimwa wala hajawahi kuvipigania). Kitendo
hicho cha kutowashirikisha wanachama na kuwanyima haki yao ya kikatiba ya
kuchagua na kuchaguliwa kilidhihirisha usaliti wa hali ya juu wa misingi ya
demokrasia
- CHADEMA watuambie njia iliyotumika kuwapata
wabunge wa viti maalumu. Ni demokrasia gani inayotoa fursa kwa baadhi tu ya
viongozi kuteua wabunge ambao wanakiwakilisha chama chote. Ambapo kila kiongozi
aliteua maswahiba zake na wengine kwa ugeni wao ndani ya CHADEMA walikosa watu
wanaowafahamu na kuamua kuwateua wanawake maswahiba wao ndani ya CCM. Msingi wa
kawaida wa kupata wabunge wa viti maalumu ukiacha kura za maoni, kigezo kingine
muhimu ni mchango wa mgombea / mwanachamahuyo katika kukijenga na kukitumikia
chama chake. Yaliyotokea kwa CHADEMA kwenye wabunge wake wa viti maalumu ni
mapya kwenye ulimwengu wa demokrasia. Inahitaji wataalamu wa sayansi ya siasa
kufanya utafiti wa aina hii mpya ya demokrasia
Tulidhani baada ya mwaka mmoja kupita, wenzetu hawa
wangelikuwa wamejifanyia tathimini, kujikosoa, kujisahihisha, na hata kufanya
uungwana wa kuwaomba radhi wanachama wao kwa uvunjifu mkubwa wa misingi ya
demokrasia, katiba na kanuni za vyama vyao
Tunatoa wito kwa vyama vya siasa nchini
kutokuchukulia kwa wepesi masuala ya demokrasia na mabadiliko, yasiwe ni nyimbo
za kuburudisha au kutoa matumaini hewaq kwa wanachama na wananchi. Kanuni
mojawapo ya demokrasia ndani ya vyama ni lazima ionekane katika muundo wake na
katika utekelezaji wa muundo huo
Umefika wakati vyama vya siasa vinapaswa kujifunza
kuuza sera ili kujenga na sio kusubiri matukio kwa ajili ya kupata huruma ya
wananchi. Tunasubiri kushuhudia na kusikia demokrasia demokrasia
itakavyoendeshwa katika uchaguzi wa ndani wa vyama hivyo ambapo kuna taarifa
mmoja wa vigogo amefanikiwa kupata kiasi cha dola milioni 15 zitakazomsaidia
kupanga safu yake ya uongozi
Katika kutimiza mpango huo, tayari yapo mawasiliano
ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi wakitoka Zanzibar na sehemu zingine za
nchi kuja Dar es Salaaam, na imeonekana dhahiri mazungumzo yao kutowashirikisha
viongozi wenzao waandamizi kwani yanalenga kafanikisha mpango huo.
Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli, ameendelea
kufanya juhudi kubwa katika kujenga nchi kwa kuimarisha utendaji na nidhamu ya
utumishi serikalini, kukusanya mapato na kusimamia matumizi sahihi ya fedha,
kupambana na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na kusimamia haki, usawa na wajibu
kwa raia. Mwenzetu anayaona haya kuwa ni kuufanya utumishi wa umma kaa la moto.
Juhudi hizi na nyinginezo ikiwemo ununuzi wa ndege
mpya, ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, afya na kununua vitanda vya
wazazi, kutoa elimu burekuanzia shule ya msingi mpaka sekondari na nyinginezo
hazipaswi kukatishwa tama kwa maslahi ya wachache ni vyema kuziunga mkono kwa
maslahi ya taifa letu
Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Rais Dk.
Magufuli madarakani, CCM inawaomba wananchi kuendelea kummunga mkono katika
dhamira yake safi yakuwaondolea kero, kuboresha huduma za jamii na kuwaletea
maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na;-
CHRISTOPHER OLE SENDEKA
MJUMBE WA NEC NA MSEMAJI WA CCM
28/10/2016