SAKATA LA SUMAYE KUNYANG'ANYWA MALI ZAKE NA SERIKALI,LAFIKIA PATAMU,MWENYEWE AIBUKA NA KUMLIPUA WAZIRI WA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
Siku moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kutangaza nia ya Serikali kumnyang’anya
shamba Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwanasiasa huyo mkongwe amedai
hilo halimtikisi.
Sumaye ambaye tayari ameshakabidhiwa notisi ya siku
90 kutokana na kutoliendeleza, amesema kuwa tayari suala hilo ameshaliwasilisha
mahakamani na kwamba mwanasheria wake ndiye anayefahamu tarehe iliyopangiwa
kesi hiyo.
“Nilienda mahakamani na ikaamuriwa kusiwe na
shughuli yoyote, nasubiri tarehe ya kesi ambayo mwanasheria wangu ndiyo
anaijua,” Sumaye anakaririwana MwanahalisiOnline.
Mwanasiasa huyo aliyehamia Chadema miezi michache
kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, amesema kuwa kama CCM wanataka
kumdhoofisha kwa kumnyang’anya mashamba ili arejee haitawezekana.
“Kama walidhani kwa kunifanyia hivi nitarudi Chama
Cha Mapinduzi (CCM) wasahau, hata kama nilikuwa na nia hiyo sirudi,” amesema
Sumaye.
Serikali imetangaza kuanza mchakato wa kumnyang’anya
Sumaye shamba lake lililoko Mwabwepande jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa
ameshindwa kuliendeleza kwa muda mrefu, kinyume na matakwa ya sheria.