Zinazobamba

AMANA BENKI YAZINDUA HUDUMA YA KUKUSANYA NA KUGAWA ZAKAT


Mkurugenzi wa Amana Bank Dk Muhsin Masoud (Kushoto)akizindua huduma ya kukusanya na kugawa zakat iliyofanyika jana katika tawi la makao Makuu Ohio Street Jijini Daresalaam. Kulia ni Naibu katibu Mkuu wa Baraza la Sunna Tanzania (BASUTA) Sheikh Muhamadi Issa (Katikati) na Dr. Abdallah Tego wakishiriki katika uzinduzi huo.

Mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mussa akifafanua huduma mpya ya kukusanya na kugawa zakat inayotolewa na Benki ya Kiislamu ya Amana. Dassu amesema huduma hiyo imeanzishwa ili kukidhi mahitaji ya soko.
 





Benki ya Kiislamu ya Amana Benki imezindua huduma mpya ya kukusanya na kugawa zakat kwa wateja wake na wale wasio wateja, dhamira ikiwa ni kuwawezesha Waislamu kutimiza kwa urahisi wajibu wao wa kutoa zakat kama nguzo ya tatu katika nguzo tano za Uislamu inavyosema.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika Hafla ya uzinduzi wa Huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt Muhsin Masoud amesema wameshawishika kuanzisha huduma hiyo kutokana naa Jamii kuhitaji chombo.

Amesema Kwa muda Mrefu kumekuwa na ombwe la chombo hicho, na kwamba kitendo cha kuanzisha huduma hiyo kutakata kiu ya muda mrefu ya Waislamu wengi. Akizungumzia kujipanga kuhusu kutoa huduma iliyo bora, Dk Masoud Amesema kupitia bodi ya Usimamizi wa Sharia watahakikisha huduma inayotolewa ni ya kiwango cha juu na yenye uwazi.

Aidha akizungumzia kuhusu ulazima wa kutumia huduma hiyo, Dkt Masoud amesema hutuma hiyo ni ya kujitolea(Hiari) Wateja hawalazimishwi kutoa zakat bali watakachokifanya ni kuwakumbusha wateja juu ya jukumu lao la kulipa zakat kulingana na kipato chao.

Naye Meneja Masoko wa Amana benki amewashauri Waislamu wakiwamo wateja na wasiokuwa wateja wa Benki ya amana kupitia Tovuti ya Benki hiyo ili kuweza kukokotoa vipato vyao na kuona kama wanauwezo wa kulipa zakat au la kwani wameweka kikokoto kitakachowasaidia kukokotoa vipato vyao.
"Tovuti ambayo wanaweza kutembelea ni ''WWW.AMANABANK.CO.TZ/SW/akaunti ya akiba binafsi/zakat service. baada ya kutambua kiasi wanachopaswa kutoa kama zakat wanaweza kulipia kupitia katika akaunti maalum ya zakat(0021104755200001) au kwa njia ya simu.