Zinazobamba

YANGA WAKUBALI KUYAISHE KWA KOCHA WAKE,WAMTUMIA WAZIRI MWIGULU KUMWOKOA KOCHA WAKE,SOMA HAPO KUJUA



 plujim

Waziri wa Mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba amefanikisha kumrejesha KochaYanga Hans Van Der Pluijm ambaye alitangaza kujiuzulu kuiongoza timu hiyo mapema wiki hii.

Katika Mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu,Mchana huu Mwigulu amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.

Hii ni mara ya pili kwa Mh.Mwigulu anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya klabu ya Yanga kwani msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga.

Ikumbukwe kuwa Mwigulu Nchemba ni mdau wa michezo nchin na mpenzi wa soka na mwanachama hai wa jangwani “Yanga”

Tazama hapo Barua kutoka kwenye Uongozi wa Yanga.

 url