Zinazobamba

TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA NCHINI INDIA.SOMA HAPO KUJUA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9sH1dmsPUgQ9bhFLYkzNmKpMwRHiBf4AGwCRyQU3vUBvUd-9iufuQmH9dBW8ufZ5OqoRZjKALHGZF5Z_QVfStYDfC6raSDx9hbYhi8NiR-irWxF4M3isf1DC6z1lDSVQVRgsEOTOHSpk/s1600/1.jpeg

Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya akizungumza na waandishi wa habar juu ya Mashindano hayo yatakayo fanyika nchini India mapema leo jijini Dar es salaam.
Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habar kuhusiana na Michuano hiyo leo jijini.
Timu ya  taifa ya michezo ya kabbadi nchini tanzania inatarajiwa kushiriki kombe  la dunia la michezo ya kabaddi yatakayoanza rasmi novemba mwaka huu  katika jimbo la punjab.

Hayo yamebainishwa na balozi wa india  nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam na kueleza kuwa mchezo huo utashirikisha
jumla ya watu 34 kati yao ikiwa ni timu ya wanawake na timu ya wanaume  pamoja na makocha wa nne.

"Tunafuraha kwa nchi ya tanzania kupata
washiriki watakaoenda nchini india kushiriki kombe hilo la dunia la kabadi wanaume wakiwa kumi na tano na wanawake kumi na tatu wakiongozwa  na makapteni wao.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi idara ya
maendeleo ya michezo,Alex NKenyenge ameongeza kuwa serikali ya Tanzania  itazidi kutoa ushirikiano na nchi hiyo hususani katika michezo ya jadi huku akizitaka timu hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ili kuipeperusha bendera ya Tanzania.
"Michezo isiishie hapa hasa hii ya jadi bali ipewe kipaumbele zaidi iweze kufika mbali na hvyo viongozi wasing'ang'anie michezo iliyozoeleka"aliongeza kaimu mkurugenzi .

Kabaddi ni mchezo maarufu katika jimbo la punjab na mikoa mingine ya india ambapo hii ni mara ya sita kufanyika kwa kombe la dunia la mchezo huo  ambapo kwa mwaka huu timu 13 kutoka sehemu mbalimbali za dunia zitashiriki ambazo ni Tanzania,USA,England,Kenya,India,Mexico n.k.