SERIKALI YAKUBALI YAISHE,YAAMUA KUREJESHA SH 8500 KWA WANAFUNZI,SOMA HAPO KUJUA
Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
imetuliza hasira za wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kurejesha posho ya chakula na
malazi ya Sh8,500 kwa kila mmoja na kwamba tofauti baina yao itakuwa viwango
vya ada.
Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali.
Ufafanuzi huu uliotolewa jana usiku na Waziri wa Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati akizungumza katika mahojiano maalimu na kituo cha runinga cha Taifa -TBC utakuwa faraja kwa wanafunzi ambao chini ya Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso) walipanga kushinikiza walipwe posho ya Sh8,500 kwa siku kama ilivyokuwa awali.
Hatua ya wanafunzi kujenga umoja ili kushinikiza
haki katika posho ilitokana na baadhi yao kuingiziwa kati ya Sh40,000 na 70,000
badala ya Sh 510,000, hali ambayo ilizua sintofahamu.
Ndalichako alisema tofauti ya malipo itakuwa katika
ada na siyo posho, “Vigezo vya mikopo vimebadilika, kila mwanafunzi atapata
fedha tofauti lakini tumefanya marekebisho kwenye posho ya chakula ambayo kila
mwanafunzi atalipwa Sh8,500 kama awali.”
Kwa mujibu wa utaratibu wa Bodi hiyo, malipo hayo ya
chakula na malazi hutolewa kila baada ya miezi miwili.
Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo.
Mapema jana, Daruso iliwataka wanafunzi wa chuo hicho kutotia saini fomu za fedha za mikopo yao mpaka itakapowapa ruhusa ya kufanya hivyo.
Rais wa Daruso, Erasmi Leon alisema hayo jana wakati
akizungumza na wanafunzi wenzake kuhusu kusudio la kwenda HESLB kwa ajili ya
kutafuta haki yao ya msingi.
“Ninachowasihi tuwe pamoja. Tuwe wamoja
na twende pamoja. Tutakwenda wawakilishi kutafuta nafasi kwa amani waweze
kusikia tuna hoja gani lakini tukinyimwa hii nafasi tutaenda kuitafuta tukiwa
wengi,” alisema na kuongeza:
“Tuwe watulivu kwa sasa
tutakapowahitaji muda na wakati wowote kwa lolote tushirikiane ili twende
pamoja tumalize pamoja tuhakikishe tunapata Sh8,500 kwa kila mwanafunzi kwa chakula
na malazi,” alisema.
Kuhusu suala hilo, uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) ulisema wajibu wake ni kupokea na kusambaza majina na taarifa
kutoka Bodi kwa wanafunzi.
Akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi waliofika ofisini
kwake kujua hatima yao na waliopata mikopo kuchukua fomu za kutia saini, Ofisa
Mikopo wa UDSM, Lugano Mwakyusa alisema wenye jukumu la kujua walio na sifa ya
kupata mikopo ni Bodi ya Mikopo.
“Tunaendelea kupokea majina kutoka bodi.
Tayari hapa kuna majina 949 yameshatoka, wengine tuzidi kusubiri na wale mwaka
wa pili na tatu ambao walikuwa na mitihani ya marudio taarifa zao zitapelekwa
bodi,” Mwakyusa aliwaambia wanafunzi waliokuwa wamejaa
ofisini kwake.
Kulikuwa na hali ya sintofahamu chuoni hapo
jana baada ya wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza kuonekana wakiwa wameshika
bahasha za kaki zilizokuwa na fomu za usajili wanazotakiwa kujaza huku
wakihangaika kutokana na kutojua kiasi cha mkopo.
Juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, AbdulRazaq Badru
alieleza kwamba ingawa wanafunzi 88,000 waliomba mikopo kutoka HESLB, uwezo wa
bodi hiyo ni kutoa kwa wanafunzi 21,500 pekee sawa na asilimia 24 na waliokuwa
wameshapatiwa walikuwa 11,000 sawa na asilimia 12.
Takwimu hizi zinaonyesha zaidi ya robo tatu ya
wanafunzi wanaohitaji mikopo watakosa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.