RAIS SHEIN AANZA KUWANANGA WAHISANI,AJITAMBA KUONGOZA NCHI BILA WAHISANI,SOMA HAPO KUJUA
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema
serikali ipo madhubuti katika kupembua misaada ambayo wahisani mbalimbali wapo
tayari na katika misaada ambayo itakuwa na masharti magumu kwa sasa serikali
haipo tayari kuipokea kwa manufaa ya wananchi.
Dkt. Shein aliyasema hayo juzi katika sherehe
za kilele cha mbio za Mwenge zilizofanyika kitaifa katika mkoa wa Simiyu na
kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na taasisi binafsi pamoja na mamia ya
wananchi pamoja na watoto wa halaiki waliopamba shughuli hiyo.
“Serikali kwa sasa tumejipanga vizuri
hatutakubali misaada yenye masharti magumu na wahisani ambao wanataka kufanya
hivyo wakae na misaada yao tutajitegemea wenyewe” Alisema
Dkt. Shein.
Aidha Rais Dkt. Shein aliwataka watanzania kuendelea
kuiunga mkono serikali kwa kuwa imedhamiria kufanya kazi kwa juhudi zote na
kusema kwamba ambao wamezoea kuchukua rushwa ni bora waache kwa kuwa serikali
haitawavumilia.
Mbio za Mwenge mwaka huu zilifikia tamati baada ya
kukimbizwa katika mikoa 31, halmashauri 179 na siku 179 ambapo zimezindua
miradi 1,387 yenye thamani ya shilingi bilioni 498.8.
Mbio za Mwenge wa Uhuru mwakani zitazinduliwa mkoani
Katavi na kuzimwa mkoani Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.