RAIS MAGUFULI AWATENSA MADEREVA WA SERIKALI,WENGI WAANZA KULIA NAYE,SOMA HAPO KUJUA
Madereva na Wasaidizi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa
Wilaya mbalimbali nchini ambao walikuwa tayari wamefika Mkoani Simiyu kushiriki
sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wameeleza kuumizwa na agizo la kurejesha
fedha za kujikimu ambazo kiasi walizitumia kwa shughuli husika.
Walisema kuwa agizo hilo la Rais John Magufuli kwao
limewatengenezea tatizo lingine la kiuchumi kwani liliwafikia kwa kuchelewa.
Baadhi yao wamesema kuwa wao hawana uwezo wa
kurejesha fedha hizo kwani hawakuomba kufanya safari hizo bali ilikuwa sehemu
ya kazi zao na kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi
kuwawezesha kufika na kuishi katika eneo hilo.
”Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za Mbio
za Mwenge wa Uhuru. Tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu
wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwa sababu ilibidi tule na kulala kwenye
nyumba za wageni. Hapo sisi kosa letu liko wapi?” Alihoji mmoja kati ya
madereva aliozungumza na gazeti la The Citizen.
Alisema kuwa anadhani uamuzi wa wao kurejesha fedha
zote ambazo tayari wamezitumia hautawatendea haki kutokana na matumizi husika
waliyofanya.
Naye msaidizi wa Mkuu wa Mkoa mmoja ambaye hakutaka
kutajwa, alisema kuwa yeye hataweza kurejesha fedha hizo kwa sababu baada ya
kufika Bariadi alilazimika kulipia chumba siku 7 alizopaswa kukaa hapo kutokana
na upungufu wa vyumba.
”Ilinibidi nimlipe mwenye chumba gharama zote za
siku 7 ambazo nilitarajiwa kuishi hapa kama nilivyotumwa kwa sababu ya uhaba wa
vyumba hapa. Sasa naanzaje kumwambia mwenye anirudishie pesa yangu yote ili
nirejeshe ofisini?” Alihoji.
Hata hivyo, wakati wasaidizi wa vigogo hao
wakionesha kuchanganyikiwa na agizo hilo ambalo wanaamini sasa linaweza
kuwaingiza hasara ambayo imetokana na kutumwa wafanye wajibu wao, baadhi ya
wakuu wa mikoa tayari wameshaanza kurejesha fedha hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ni mmoja kati
ya wakuu hao wa mikoa walioweka wazi mbele ya waandishi wa habari kusitisha
safari hiyo na kurejesha kiasi cha fedha walizopangiwa kwa shughuli hiyo.
Rais John Magufuli aliagiza viongozi wote pamoja na
wasaidizi wao waliokuwa wamepanga kuhudhuria sherehe za kuzimwa kwa mbio za
Mwenge mkoani Simiyu wasitishe safari zao na waliokwishachukua posho
wazirejeshe