PAUL MAKONDA AFANYA TUKIO HILI LA MFANO MKOA WA DAR ES SALAAM,SOMA HAPO KUJUA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wakazi
wa Mkoa wa Dar es Salaam kutunza mazingira hasa sehemu zenye mazalia ya mbu ili
kuepukana na ugonjwa wa mabusha na matende.Makonda ametoa wito huo siku ya leo.
Kata ya Buguruni
wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji unywaji dawa na kufanyiwa upasuaji kwa
magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambayo ni Matende, Mabusha, Kichocho, Minyoo na
Usubi, ambapo takwimu zinaonesha wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa
wakisumbuliwa na magonjwa ya minyoo, matende na mabusha.
Makonda ameeleza ni vyema wakazi wa Dar es Salaam wakaitumia
fursa hiyo ya kampeni itakayodumu kwa siku tano kuanzia siku ya leo mpaka
Oktoba 30, kwani kujitokeza kwao kwa wingi kupimwa na kunywa dawa kutaisaidia
serikali kuinua nguvu kazi itakayochochea ukuaji wa uchumi kwani watu wakiugua
maradhi hayo bila ya kupata tiba au kuwa na kinga mapema hupoteza nguvu kazi.
Makonda ameongeza kuwa takribani ya watu 6400 wamegundulika
na mabusha hivyo ni vyema wakawahi mapema na wengine wajitokeze kwa wingi
kuizidi idadi ya wananchi milioni 3.9 waliojitokeza mwaka 2009.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Grace
Maghembe amewataka wakazi hao kutosikiliza upotoshaji wa kuwa wakitumia dawa
hizo hawatakuwa na uwezo wa kupata watoto na badala yake wajitokeze kwa wingi
kwani dawa hizo ni salama, huku akisisitiza kuwa kwa zoezi la unywaji wa dawa
litaishia Oktoba 30 huku upasuaji ukiendelea mpaka mwezi Desemba ambapo tayari
upasuaji kwa watu wenye mabusha unaendelea kwa kituo kilichopo Pugu na zaidi ya
watu 76 wamepatiwa matibabu katika kituo hicho, ambapo hapo baadae wataongeza
vituo vingi zaidi kwa maeneo mengine.