NIA YA TAMWA KUHUSU MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WANAHABARI
Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania -TAMWA kimeamua kuungana na
Watanzania, Serikali na wadau wote katika kupambana na ajali za
barabarani zinazoweza kuzuilika, ili kuokoa vifo vya watanzania baada
kuanza utekelezaji wa mradi wa usalama barabarani.
Mradi wa usalama barabarani una lengo kubwa la kuona kwamba, wanahabari
wanapata weledi wa kuandika habari hizi kwa mapana yake, lakini hasa
kwa kuzingatia kuwa wanatoa elimu kwa jamii ya Tanzania kuhusu masuala
ya usalama barabarani.
Kwa kuanza TAMWA imeendesha mafunzo ya siku tatu
kwa wanahabari ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuandaa habari hizi.
Awamu ya pili na tatu ya mafunzo itafuatia siku chache zijazo.
TAMWA inaamini kuwa wananchi wengi watapokea elimu hii kwa kusoma habari
katika magazeti, na kusikiliza Radio na hata kuona vipindi mara kwa
mara kutoka kwenye televisheni.
Kutokana na idadi kubwa ya vifo vinavyosababishwa na ajali
za barabarani, ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini.
TAMWA
inaona kuna umuhimu wa kuvalia njuga suala hili kwa kushirikiana na
wenzetu (wadau) kama vile wanasheria kwa kuzifanyia marekebisho sheria
na kanuni za usalama barabarni ili kuipa nguvu 'Sheria ya Usalama
Barabarani ya mwaka 1973’, sheria ambayo kwa njia moja au nyingine
itaweza kudhibiti watumiaji wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara.
Maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni; mwendo kasi,
ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na
vizuizi kwa watoto.
TAMWA inatambua kwamba wanawake wengi na watoto ndio wenye kubeba mzigo
mkubwa unaotokana na ajali barabarani, ingawa takwimu zinaonyesha kuwa
waathirika wa juu wa usalama barabarani ni wanaume.
Ila ukweli ni
kwamba wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi kwani watoto hukosa
huduma na mahitaji ya msingi baada ya kupoteza watu wanaowategemea