Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada
zilizokuwa zikitolewa na Wakufunzi wa mafunzo hayo Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
Takriban
asilimia 85 ya nchini zote duniani zimegundulika kuwa hazina sheria
madhubuti za kuondokana na ongezeko la vifo vinavyotokana na ajali za
barabarani.
Takwimu
hizo ni Kwa mujibu wa Tafiti zilizofanywa na shirika la afya Duniani
WHO mwaka 2015 ambapo imebainika kuwa takriban vifo million 1.25
hutokea kila mwaka dunia kutokana na ajali za barabarani ambapo Afrika
inaongoza kwa asilimia kubwa.
Akizungumza
katika semina ya usalama barabarani ambayo iliandaliwa na chama cha
waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) Mkurugenzi wa chama hicho
Mama Edda Sanga amesema kuwa hali bado si nzuri katika suala zima la
usalama barabarani.
“Kwasasa
kuna ajila nyingi zimepitiliza duniani ambapo zaidi ya majeruhi million
20 hutokea kila mwaka kwa ajali za barabarani ambapo nchi za afrika
zinaongoza kwa asilimia 90 na hiyo inatokana na na kutokuwa na sheria
ya usalama barabarani iliyo madhubuti”.
Kwa
upande wake Mary Richard ambaye ni wakili Toka Chama cha sheria
wanawake Tanzania TAWLA lisema kuwa sheria iliyopo ya usalama barabarani
ya mwaka 1973 bado haihamasishi kufanya vizuri katika eneo hilo kwani
haijaweka mkazo katika mambo mbalimbali.
“Sheria
yetu ya usalama barabarini imekuwa na mapungufu mengi ambayo
inampelekea mtekelezaji kushindwa kuitekeleza kama suala zima la uvaaji
wa kofia ngumu(HELMET)kwa waendesha bodaboda haimemtaka mwendesha
bodaboda pekee kuvaa kofia lakini si abiria jambo ambalo ni hatari kwa
jamii”.
Hata
hivyo wananchi nao wameweza kutoa Maoni yao kuhusiana na sheria hiyo
ya Usalama barabarani ya Mwaka 1973 ambapo wameunga mkono ubadilishwaji
wake na kutaka kuangalia namna ya Kuiweka ili ajali za barabarani ziishe
ifika 2020,John Mark alisema kuwa sheria bado haipo wazi hasa suala
zima la utumiaji simu wakati wakuvuka barabara na kuendesha gari hivyo
bila kuziangalia kwa mapana zaidi haiwezi kulinda usalama wa wananchi”
Je
nini jitihada za wadau wa kisheria katika suala zima la sheria hii ya
usalama wa barabara katika kuihamasisha serikali kuboresha sheria
hiyo,wakili wa huduma za msaada wa kisheria TAWLA ,Mary.anaeleza
“Alisema kuwa eneo lao kubwa wao ni kushawishi na kutoa elimu kutokana na utaratibu wa kubadilisha sheria ni serikali na Bunge”.
|