NCHI INAUPUNGUFU WA DAWA HII,MAKAMU WA RAIS AKUBALI KUSEMA KWELI,SOMA HAPO KUJUA
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amekiri
kuwapo uhaba wa dawa na vifaa tiba katika hospitali za Serikali
nchini.
Amesema uhaba huo wa dawa ni changamoto ya muda
mfupi na Serikali inatafuta ufumbuzi wa haraka kuwahudumia wananchi.
Alikuwa akizungumza Dar es Salaam jana wakati
akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya kina mama na watoto katika hospitali
zote za rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam.
Samia alisema anatambua changamoto zinazoikabili
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwamba ni ukosefu
wa dawa.
“Natambua katika hospitali zetu za rufaa
tuna changamoto ya vifaa tiba na dawa, lakini Serikali tunaifanyia kazi
kila mwananchi aweze kupata huduma hizo kama ilivyopangwa,”alisema.
Alisema idadi watu wanaoongezeka katika
Mkoa wa Dar es Salaam husababisha msongamano wa wajawazito na watoto katika
hospitali za Serikali na kuwafanya kina mama walale chini au walale mbali na
watoto wao.
“Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni,
takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000, hufa kila mwaka kutokana na uzazi
na asilimia 80 ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, umbali wa
vituo vya afya, upasuaji wa huduma za dharura ya upasuaji kwa wajawazito na
kuongezewa damu.
“Kwa Mkoa wa Dar es Salaam peke yake,
kuna zaidi ya hospitali 42 zinazotoa huduma za dharura za uzazi kwa kasi ya
ukuaji wa jiji na bado Serikali inahitaji zaidi ya hospitali 30 ndani ya miaka
10 ijayo,”alisema.
Kwa mujibu wa Samia, mradi wa ujenzi huo utagharimu
Sh bilioni 4.5 kwa hospitali tatu na kila hospitali yenye ghorofa tatu na
uwezo wa kuwekwa vitanda 150, itagharimu Sh bilioni 1.2.
Alisema Serikali imejipanga kuhakikisha hospitali
zote za rufaa zinaendelea kuimarishwa ili kutoa huduma bora za afya ikiwamo
afya ya mama na mtoto